RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akisoma Jiwe la Msingi la Jengo la ZURA Maisara, baada ya kuweka jiwe hilo, ikiwa ni shamrashamra za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, hafla hiyo imefanyika leo, 6-1-2019, katika eneo hilo maisara.
RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AWEKA JIWE LA MSINGI JENGO LA ZURA MAISARA ZANZIBAR
Matokeo ChanyA+
January 7, 2019
Taarifa Vyombo vya Habari , Taarifa ya Habari , Tanzania MpyA+
769 Imeonekana
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akitembelea jengo hilo la ZURA, baada ya hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi la jengo hilo, akipata kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa ZURA Ndg.Haji Kali Haji, kulia na kushoto Waziri wa Ardhi,Nyumba,Maji na Nishati Zanzibar Mhe. Salama Aboud Talib, akitembelea jengo hilo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoa kipazia kuashiria kuweka Jiwe la Msingi la Jengo ZURA Maisara Zanzibar, ikiwa ni shamrashamra za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar, kulia Waziri wa Ardhi, Nyumba,Maji na Nishati Zanzibar Mhe. Salama Aboub Talib, akishuhudia uwekaji wa jiwe la msingi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla ya Uwekaji wa Jiwe la Msingi la Jengo la ZURA Maisara Zanzibar ikiwa ni shamrashamra za kuadhimisha Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Jengo Jipya la ZURA Zanzibar linalojengwa katika eneo la maisara litakuwa na gorofa saba pacha. litakapomalizika ujenzi wake unaojengwa na Kampuni ya Kichina ya Hainan International Ltd.
Ad