MATIBABU YA MOYO INAYOFANYIKA KATIK TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE KUANZIA TAREHE 7/01/2019 HADI 18/01/2019
Taasisiya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kupitia madaktari wake bingwa wa magonjwaya moyo kwa kushirikiana na Madaktari Afrika na Shirika la Cardio Startwote kutoka nchini Marekani wameanza kambi maalum ya matibabu ya moyoya siku 12 kwa watu wazima .
Matibabu yanayofanyika katika kambi hiyo ni upasuaji wa kufungua kifua na bila kufungua kifua. Upasuaji wa bila kufungua kifua unafanyika kupitia tundu dogo linalotobolewa kwenye paja kwa wagonjwa kuzibuliwa mishipa ya moyoiliyoziba (Percutaneous Coronary Intervention – PCI) na kuwekewa vifaa vinavyosaidia kurekebisha mapigo ya moyo ambavyo ni (Permanent Pacemaker na High powered devices CRT-P, CRT –D) .
Wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji ni wale wenye matatizo ya moyo ambayo ni valve, mishipa ya moyo iliyoziba, moyo kushindwa kufanya kazi vizuri, matibabu kwa watu wazima waliozaliwa na matatizo ya moyo na wale wenye matatizo ya moyo yaliyotokana na ugonjwa wa Kisukari
Kambi hii inaenda sambamba na utoaji wa elimu kwa madaktari na wauguzi pamoja na kubadilishana ujuzi wa kazi kwa wageni na wataalamu wetu. Katika kambi hii tunatarajia kufanya upasuaji wa kufungua kifua kwa wagonjwa 20 na bila kufungua kifua kwa wagonjwa 25. Hadi leo tarehe 8/1/2019 jumla ya wagonjwa nane wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua na wagonjwa wanne wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua.
Hii ni kambi ya kwanza ya matibabu ya moyo tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2019 na ni mara ya kwanza kwa shirika Cardio Start kuja hapa nchini kufanya kazi na sisi.
Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
08/01/2019