- Hospitali ya Magonjwa ambukizi Kibong’oto inayotoa huduma ya Kifua Kikuu ‘TB’ na magonjwa mengine ya kuambukiza hasa UKIMWI imeendelea kutoa huduma bora kutokana na serikali kuwekeza katika ununuzi wa vifaa vya kisasa vya uchunguzi na tiba.
- Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo Dkt.Riziki Kisonga wakati akizungumza na maofisa habari na uhusiano wa wizara na taasisi walofika hospitalini hapo katika kampeni ya “Tumeboresha Sekta ya Afya” ambayo inaelezea mafanikiao ya miaka mitatu inayofanyika katika sekta hiyo.
- Dkt.Kisonga alisema kuwa ununuzi wa vifaa hivyo umeweza kurahisisha utoaji wa huduma katika hospitali hiyo.
- Aidha, alisema katika kufanya kazi na jamii ya wachimbaji wadogo wadogo kutoka machimbo ya Tanzanite Mererani,kumekuwepo na idadi kubwa ya wanaougua ugonjwa wa kifua kikuu.
- “Ufuatiliaji uliofanywa unaonyesha maambukizi ya TB katika jamii hiyo ni mara kumi na tano(15) zaidi ikilinganishwa na jamii isiyofanya kazi katika machimbo”.Alisema Dkt.Kisonga
- Alisemaa hospitali yake imeendelea kutoa elimu ya kujikinga na vumbi ambayo ni chanzo kikubwa cha uharibifu wa mapafu hivyo kufanya iwe rahisi kwa jamii ya wachimbaji wadogo wadogo na familia zao kupata maambukizi ya mimelea vya ugonjwa wa kifua kikuu.
- Hata hivyo Serikali imenunua mashine ya zinazorahisisha ugunduzi wa haraka wa vimelea hivyo katika muda wa masaa mawili na mara wanapogundua wanaanza tiba mara moja.
- Dkt.Kisonga amesema katika kukabiliana na changamoto hiyo pia wameanzisha kituo cha afya Mirereni ambacho kinatoa huduma za matibabu ya TB.
- “Tumenunua mashine za kisasa zenye thamani ya Sh. 201 ambazo zina uwezo wa kubaini kifua kikuu ambacho hakijaanza kuwa na dalili zilizozoelekea na kubaini usugu wa dawa kwa mgonjwa ambaye haponi licha ya kutumia dawa,” alisema Dk. Kisonga
- Amesema hospitali hiyo kwa sasa ina wagonjwa waliolazwa123 na kati yao wagonjwa 86 ni wagonjwa wa kifua kikuu sugu
- Aidha, kutokana na kuboresha huduma ya matibabu ya TB, serikali imeanzisha huduma za kifua kikuu sugu katika hospitali za serikali kwenye mikoa nchini na hivyo hospitali hiyo kupokea wagonjwa sugu na wanaohitaji uchunguzi zaidi.
- Pia alisema wana mpango wa kuanzisha maabara inayotembea ili kufika kwenye jamii kwa ajili ya kutoa elimu na kufanya vipimo.
- Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Dunuani (WHO) watu 246 kati ya watu 100,000 wanaugua TB duniani.
Ad