- Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dokta Mary Mwanjelwa amesema wizara ipo katika hatua ya mwisho ya kuwa na mfumo mpya wa kupata taarifa za watumishi wa umma kote nchini ikiwa ni pamoja na kituo cha kutoa huduma kwa pamoja.
- Naibu Waziri Mwanjelwa amesema hayo katika mahojiano katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na TBC ambapo amesema kuwa mfumo huo utawezesha kupatikana kwa taarifa za watumishi kwa urahisi.
- Katika hatua nyingine Dokta Mwanjelwa amewataka waajiri kuwa na utaratibu wa kupeleka taarifa zilizo sahihi kuhusiana na watumishi wao ili kuondoa ucheleweshwaji wa kupanda madaraja kwa watumishi.
- Amesema mara nyingi wizara imekuwa ikilaumiwa kutokona na ucheleweshwaji wa masuala mbalimbali jambo ambalo huanzia katika ofisi zao na kuwataka waajiri kubadilika.
- Msikilize Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dokta Mary Mwanjelwa akitoa ufafanuzi
Ad