- Uwekezaji uliofanyiwa katika mradi wa uchimbaji madini ya uranium katika mto Mkuju ulioko mkoani Lindi ya Uranium One umefikia kiasi cha dola za kimarekani Milioni mia mbili ($200mil) toka mradi ulipoanza mwaka 2009.
- Akizungumzia na Waziri wa Madini Dotto Biteko mjini Dodoma, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Uranium One, Frederick Kibodya amesema manufaa ya mradi huo ni pamoja na kusaidia katika kukuza teknolojia nchini. Amesema madini hayo yakichimbwa yanatumika katika kuzalisha umeme ambayo ni teknolijia mpya nchini.
- Aidh Mkurungezi huyo amesema kuwa mradi utasaidia katika kuongeza ajira nchini na kufafanua kuwa kwa kipindi cha ujenzi wa mradi wanatarajia kuajiri watanzania 1600 kwa kipindi cha miezi kumi na nane.
- Aidha, alibainisha kuwa kutakuwepo na uzalishaji kwaajila sekta zisiso rasmi kiasi cha watu 4500 wakati wa ujenzi na 2300 pindi uzalishaji utakapoanza.
- Pia Kibodya amesema, mradi unatarajia kuliingizia taifa pato la kiasi cha dola za kimarekani milioni 220 kama kodi kwa mwaka, kiasi ambacho kitakuwa kikibadilika kadri uzalishaji unavyoongezeka.
- Mradi wa uchimbaji madini ya uranium katika mto Mkuju unafanywa kwa ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Mbia wa kampuni ya Mantra anayejulikana kama Rosatom.
Ad