MAKAMU WA RAIS – CONGO IMEANDIKA HISTORIA MPYA

  • Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Congo imeandika historia mpya kwa kukabidhiana madaraka kwa upendo na ana imani Viongozi wataendelea kufanya kazi kwa pamoja kwa ajili ya maendeleo na maslahi mapana ya nchi yao.

MAMY-2

  • Makamu wa Rais ambaye alimuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameyasema hayo mara baada ya sherehe za kumuapisha Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Felix Tshisekedi.

MAMY-1

  • “Linalofurahisha ni kwamba ni mara ya kwanza kwa nchi hii ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kufanya uchaguzi wa kidemokrasia na kukabidhiana madaraka kwa usalama kabisa” alisema Makamu wa Rais.

Msikilize Makamu wa Rais

[soundcloud url=”https://api.soundcloud.com/tracks/564273267″ params=”color=#ff5500&auto_play=false&hide_related=false&show_comments=true&show_user=true&show_reposts=false&show_teaser=true&visual=true” width=”100%” height=”300″ iframe=”true” /]
  •  Uchaguzi huo uliofanyika Desemba 30, 2018, Mhe. Felix Tshisekedi alipata takribani kura milioni 7 sawa na asilimia 38.57 ya kura zilizopigwa ambapo wagombea wenzake kama Martin Fayulu alipata ailimia 34 sawa na kura milioni 6.4, Bw. Emmanuel Ramazani Shadary alipata asilimia 23 sawa na takribani kura milioni 4.4.
  • Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeandika historia kwa mara ya kwanza tangu ilipopata uhuru kwa kukabidhiana madaraka kwa njia ya Aman
Ad

Unaweza kuangalia pia

TANZANIA YATAKA AMANI KUPUNGUZA MZIGO WA WAKIMBIZI AFRIKA

Tanzania imetaka Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada na nguvu katika kuleta …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *