Waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza wakati akitoa taarifa ya wizara ya madini kwenye mkutano wa uanzishwaji wa Masoko ya Madini uliohudhuriwa na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma

WIZARA YA MADINI YAANZA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA RAIS MAGUFULI, KUANZISHA MASOKO YA MADINI

  • Wizara ya Madini imeanza utekelezaji wa Maagizo mbalimbali yaliyotolewana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli yenye lengo la kuboresha mchango wa Sekta ya Madini.
  • Hayo yamesemwa na Waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko leo tarehe 26 Januari 2019 wakati akitoa taarifa ya wizara hiyo kwenye mkutano wa uanzishwaji wa Masoko ya Madini  uliohudhuriwa na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa,
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akiwahutubia Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara, wakati akifungua mkutano kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma
  • Amesema kuwa kwa sasa Wachimbaji na wafanyabiashara wa madini hawana maeneo maalumu wanayoweza kufanyia biashara ya madini hali ambayo imechangia kuwepo utoroshaji wa madini, hivyo kuikosesha Serikali mapato stahiki.
  • Mhe Biteko amesema kuwa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2017, kupitia Sheria ya The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Act, 2017. Maeneo muhimu katika marekebisho hayo ni pamoja na: hisa za serikali katika uchimbaji wa madini (Kifungu Na.10)
Vingozi mbalimbali wakifatilia mkutano
Vipngozi mbalimbali wakifatilia mkutano wa uanzishwaji wa Masoko ya Madini uliohudhuriwa na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma
  • Serikali kuwa na hisa zisizolipiwa zisizopungua asilimia16 katika kila Leseni za Uchimbaji Madini (Special Mining Licence na Mining Licence) na kuweza kupata hisa Zaidi hadi kufikia asilimia 55 kwa kuzingatia unafuu wa kodi aliopewa Mchimbaji, kuanzishwa kwa Tume ya Madini ili kusimamia utoaji wa leseni za utafutaji na uchimbaji wa madini na biashara ya madini; kufanya ukaguzi katika maeneo ya utafiti na uchimbaji madini; kusimamia hifadhi ya mazingira na usalama migodini.
  • Aidha, kuanzisha Masoko ya Madini (Mineral and Gem Houses) ambayo itajumuisha minada ya madini (Minerals Auction Centers) Masoko ya Madini (Minerals Exchange) na Vituo vya malipo na makabidhiano (Clearing House).
  • Vilevile, kuanzishwa kwa Akiba ya Taifa ya Madini katika Benki Kuu ya Tanzania. Akiba hiyo itakuwa sehemu ya mrabaha kwa madini yaliyosafishwa na madini yaliyokamatwa kwa mujibu wa sheria.
Waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko
Waziri wa madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza wakati akitoa taarifa ya wizara ya madini kwenye mkutano wa uanzishwaji wa Masoko ya Madini uliohudhuriwa na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma
  • Biteko amesisitiza kuwa Maeneo mengine ambayo yameguswa na Marekebisho ya sheria hiyo ni kuanzishwa kwa Maghala ya Serikali kwa ajili ya kutunzia madini ya metali na vito yaliyozalishwa nchini, ambayo inaeleza kwamba kila Mchimbaji kuwa na sehemu ya kutunzia madini katika eneo la mgodi kwa ajili ya kuhifadhi madini anayozalisha na kuweka kumbukumbu ya madini hayo.
  • Hata hivyo, Mchimbaji anatakiwa kuhamisha madini hayo kwenye maghala ya Serikali ndani ya siku tano kwa ajili ya kusubiri kusafishwa (refined) kuuzwa au kusafirishwa nje ya nchi. Madini yote kutakiwa kuongezewa thamani kabla ya kusafirishwa au kuuzwa nje ya nchi, kampuni zinazojihusisha na utafiti na uchimbaji wa madini kununua bidhaa na kutumia huduma zinazopatikana hapa nchini na kuajiri raia hasa kwa kada ambazo Watanzania wapo.
  • Kadhalika, kampuni hizo zinatakiwa kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo na huduma za jamii kama vile shule na hospitali kwa jamii inazozizunguka Kampuni hizo zinatakiwa kupanga mipango ya kuchangia miradi ya maendeleo na huduma za jamii kwa kushirikiana na Halmashauri husika. Halmashauri zinatakiwa kutoa miongozo ya kutoa huduma hizo kwa Kampuni.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Stanislaus Nyongo
Naibu Waziri wa Madini Mhe Stanislaus Nyongo akifuatilia mkutano wa uanzishwaji wa Masoko ya Madini uliohudhuriwa na Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara katika ukumbi wa Hazina Jijini Dodoma
  • Marekebisho hayo yaliyofanyika Mwaka 2017 katika Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 ili kuweza kulinda maslahi ya taifa letu na kuhakikisha kwamba Sekta ya Madini inachangia ipasavyo katika kukuza na kuimarisha mchango wa Sekta hii katika Pato la Taifa” Alikaririwa Mhe Biteko
  • Aidha, mbali na marekebisho hayo ya Sheria, tarehe 25 Februari, 2018, Mhe. Stanslaus Nyongo aliunda Kamati maalum kuangalia namna bora ya kudhibiti utoroshwaji wa madini na uanzishwaji wa soko la madini.
  • Katika taarifa ya kamati hiyo ilionekana kuwa moja ya sababu kuu inazosababisha utoroshaji wa madini ni kukosekana kwa Soko la uhakika kwa wazalishaji wa Madini hapa nchini. Pamoja na taarifa hiyo, kwa nyakati tofauti Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekuwa akitoa maagizo ya kuanzisha masoko hayo. Kati ya siku alizotoa maagizo hayo ni pamoja na alipokuwa akiniapisha kuwa Waziri wa Madini na siku alipofungua Mkutano wa Wachimbaji Wadogo na Wadau wa Biashara ya Madini uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 22 Januari, 2019. Kwa mara nyingine alirudia kauli hiyo.
  • Alisema Ili kukabiliana na changamoto ya Masoko ya Madini, Wizara ya Madini iliunda kamati iliyojumuisha wajumbe kutoka katika taasisi mbalimbali za Serikali zikiwemo Ofisi ya Rais – Ikulu, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara ya Madini, Wizara ya Fedha, Wizara ya Viwanda na Biashara, Benki kuu na Tume ya Madini. Kamati hiyo iliundwa ili kuandaa rasimu ya Kanuni za kuanzisha na kusimamia Masoko ya Madini Nchini.
  • “Kamati ilianza kutekeleza majukumu yake tarehe 15 Januari, 2019 ambapo nilikutana nayo, na pia, Mwanasheria Mkuu wa Serikali-Mhe. Adelardus Kilangi. Kwa pamoja tuliwaeleza Wajumbe umuhimu wa kanuni za kuanzisha na kusimamia masoko ya madini Nchini” Alisema na kuongeza kuwa
  • “Katika kikao hicho cha kamati nilisisitiza kufanya marejeo katika taarifa za Kamati iliyoundwa na Mhe. Stanslaus Nyongo, Naibu Waziri wa Madini na taarifa ya ziara ya mafunzo katika Nchi za India na Falme za Kiarabu kuhusiana na uanzishwaji wa masoko ya bidhaa za madini pamoja na Sheria za Madini. Mafunzo hayo yalihusisha Watendaji wa Wizara na Wataalam wengine ndani ya Serikali. Aidha, nilielekeza mambo ya kuzingatia katika uandaaji wa rasimu hiyo kuwa ni umiliki wa madini, ukusanyaji wa kodi na tozo mbalimbali, upatikanaji wa mitaji kwa wachimbaji wadogo na namna ya ushiriki wa wachimbaji wadogo katika masoko hayo. Vile vile, nilisisitiza kuwa msingi wa kanuni hizo ni kifungu cha 27C (1) cha Sheria ya Madini ya 2010.” 
  • Katika kuandaa kanuni hizo, jina la Kanuni linalopendekezwa ni The Mining (Mineral and Gem Houses) Regulations, 2019. Rasimu ya Kanuni ina sehemu kuu tano ambazo zitaelezwa wakati wa kutoa mada hii.
  • Waziri Biteko amewaomba Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Maafisa Madini Wakaazi wa Mikoa na Wadau kwa ujumla kufanya kazi kwa pamoja ili kutimiza ndoto za muda mrefu za Wachimbaji wadogo, wafanyabiashara wa Madini, Wadau na Watanzania wote kwa ujumla.
  • Mhe Biteko amesisitiza, viongozi hao kuendelea kumuunga mkono kwa juhudi na bidii kubwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye anataka kuona Sekta hiyo inawanufaisha Wachimbaji wadogo na Watanzania wote kwa ujumla.
  • Mkutano huo umefunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SOKO LA MDINI ULANGA LA KUSANYA MILIONI 396 NDANI YA MIEZI 5

Waziri wa Madini Doto Biteko amesema tangu kuanzishwa kwa soko la madini Ulanga wamenunua madini …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *