- Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye amekabidhi kompyuta 25 kwa shule za sekondari Mpanda mkoani Katavi kwa lengo la kukuza kiwango cha ufaulu na kuongeza matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) shuleni kwa kuwawezesha waalimu kutumia kufundishia na wanafunzi kujifunzia.
- Amefafanua kuwa lengo ni kupate wanafunzi mahiri kwa kompyuta hizo kutumika na wanafunzi wengine kwenye shule mbali mbali kwa kuziunganisha kompyuta hizo kwenye mtandao ili mwalimu mmoja aweze kufundisha wanafunzi wengi wengine wa shule nyingine
- “Kumbukeni hapo zamani wanafunzi wa mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma ilikuwa inatoa wanafunzi wenye ufaulu mzuri, hivyo tuwarithishe wanafunzi wetu,” amesisitiza Nditiye
- Kompyuta hizo zimetolewa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ambao una dhamana ya kuhakikisha wananchi waishio vijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara wana wasiliana kwa kuzipatia kampuni za simu za mkononi ruzuku ya kujenga minara ili kufikisha huduma za mawasiliano maeneo mbali mbali nchini
- Nditiye amekabidhi kompyuta 25 zenye thamani ya shilingi milioni 46 kwa Mbunge wa Mpanda Mjini, Mhe. Sebastian Kapufi kwa niaba ya waalimu na wanafunzi wa shule za sekondari zilizopo mjini humo kwa kuwa aliiomba Serikali kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu ili shule hizo ziweze kupatiwa kompyuta hizo.
- “Nimeanza kumsumbua Nditiye zaidi ya mwaka mmoja na nusu kuomba kompyuta, unaweza kuona kompyuta ni chombo chepesi ila sio hivyo kwa kuwa ni chombo muhimu na kitatunza siri,” amesema Kapufi
Ad