- Wachimbaji wadogo mkoani Geita wanatarajiwa kufikishiwa Umeme katika mashimo yao ili kuwawezesha kufanya shughuli zao za uchimbaji kwa ufanisi mkubwa. Hayo yalisemwa na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Imwelu kilichopo wilaya ya Chato mkoani Geita.
- Alisema kuwa Serikali inatambua mchango wa wachimbaji wadogo katika maendeleo ya nchi na kwa sasa umeme utafikishwa katika mashimo ya wachimbaji ili kurahisisha shughuli zao za uchimbaji. “Ndugu zangu wachimbaji tumeshaanza kuwapa transfoma kwa hiyo kama wewe ni mchimbaji na unataka uchimbaji wao uwe wa kisasa,utajaza fomu itakayowezesha kuendesha mashine zenu za kuchakata madini”Alisema.
- Waziri huyo aliwasihi wachimbaji wadogo kutumia fursa ya umeme ili kuleta tija katika uchumbaji wao na hivyo kuweza kuongeza pia ufanisi mkubwa. Hata hivyo Waziri Kalemani alimtaka Mkandarasi na Tanesco kufikisha umeme katika kijiji hicho ndani ya siku ishirini (20)
Ad