TANZANIA NA KUWAIT ZAJADILI UDHIBITI WA MIPAKA

NAIBU WAZIRI MASAUNI
Balozi wa Kuwait nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni juu ya kubadilishana uzoefu katika Udhibiti wa Mipaka.Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Ofisi Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  • Serikali ya Tanzania na Nchi ya Kuwait ziko katika mpango maalumu wa kubadilishana uzoefu juu ya udhibiti wa mipaka ikiwa ni juhudi za Tanzania kuimarisha ulinzi katika mikoa yote nchini iliyopo mipakani
MASA-2
Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan akisaini Kitabu cha Wageni baada ya kuwasili Ofisi Ndogo ya Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  • Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa mazungumzo na Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan ikiwa ni mpango wa nchi hizo kubadilishana uzoefu katika kudhibiti uhalifu katika mikoa ya mipakani
  • “Kama Serikali tuna vipaumbele katika kudhibiti  mipaka yetu kutokana na uhalifu unaotokea ikiwemo wahamiaji haramu,usafirishaji wa binadamu, uingiaji wa silaha,utoroshwaji wa madini na biashara yamagendo, ndio maana tumekutana leo kujadili ushirikiano wa nchi hizi mbili katika kudhibiti uhalifu huo”alisema Masauni
MASA-4
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Balozi wa Kuwait nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan (kulia), juu ya kubadilishana uzoefu katika Udhibiti wa Mipaka. Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Ofisi Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  • Akizungumza katika kikao hicho Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan alisema Tanzania ni nchi salama na wameamua kubadilishana uzoefu katika usimamiaji na udhibiti  wa mipaka.
  • “Tuna uhusiano mzuri baina ya Kuwait na Tanzania,tumekubaliana kubadilisha uzoefu ili kuweza kuimarisha sekta ya ulinzi kwa kutumia teknolojia itakayorahisisha udhibiti wa mipaka hapa nchini Tanzania” alisema Balozi Mubarak
  • Katika mazungumzo hayo pia walijadili juu ya teknolojia ya udhibiti wa majanga ikiwemo moto na ajali ambapo pia ni eneo ambalo nchi hizo mbili zilishaanza kushirikiana katika shughuli za uokozi.
Ad

Unaweza kuangalia pia

ZOEZI LA USAJILI LA VITAMBULISHO VYA TAIFA LASHIKA KASI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *