Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya Rogers Sian’ga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kongamano linalotarajiwa kufanyika Februari 13 ambalo litawakutanisha wasanii wa fani mbalimbali nchini ili kujadili athari za dawa za kulevya ofisini kwake jijini Dar es salaam, Kulia ni Kamishna wa Kitengo cha Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi.

MAMLAKA YA KUPAMBANA NA KUDHIBITI DAWA ZA KULEVYA YADHIBITI WASAFIRISHAJI DAWA ZA KULEVYA

  • Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya Rogers Sian’ga amesema kwa sasa wamefanikiwa kidhibiti njia ambazo zilizokuwa zinatumiwa na wafanyabiashara wa dawa za kulevya kuingiza dawa hizo nchini.
  • Amesema kwa sasa njia ambayo inatumiwa na baadhi ya wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa hizo imebaki ya Kusini ambako dawa zinapitishwa kutokea nchini Msumbiji na tayari wameweka mikakati ya kuidhibiti njia hiyo.
Kamishna Jenerali
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kupambana na Kudhibiti Dawa za Kulevya Rogers Sian’ga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Kongamano linalotarajiwa kufanyika Februari 13 ambalo litawakutanisha wasanii wa fani mbalimbali nchini ili kujadili athari za dawa za kulevya ofisini kwake jijini Dar es salaam, Kulia ni Kamishna wa Kitengo cha Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Tanzania Joyce Fissoo
  • Sian’ga amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati anazungumza na waandishi wa habari kuhusu Kongamano linalotarajiwa kufanyika Februari 13 ambalo litawakutanisha wasanii wa fani mbalimbali nchini ili kujadili athari za dawa za kulevya ambapo mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan.
  • Hivyo pamoja na kuzungumzia kongamano hilo, waandishi walitaka kufahamu ni kiwango gani Mamlaka hiyo imedhibiti biashara ya dawa za kulevya nchini ambapo amejibu uingizwaji wa dawa upo lakini umepungua kwa kiwango kikubwa sana ukilinganisha na miaka ya zamani kabla ya mamlaka hiyo kuwepo.
  • “Kwanza ifahamike kuwa usafirishaji wa dawa za kulevya sio Tanzania peke yake bali lipo katika nchi mbalimbali duniani.Tunashirikiana na nchi nyingine katika kupambana na dawa za kulevya na kuna njia ya Kusini ndio imeibuka.
  • “Katika mapambano hayo katika njia ya baharini mwaka jana zimekamatwa tani 9000 kutokana na ushirikiano wa nchi mbalimbali katika ukanda wa baharini.Pia mwaka jana dawa za kulevya aina ya heroin zilikamatwa kilo 185 na sehemu chache ya dawa hizo zinakwenda Msumbiji ambazo baadae zinaingizwa nchini Tanzania,” amesema.
  • Amefafanua kwa ujumla kiwango cha uingizwaji dawa za kulevya nchini kimepungua na kwa sasa hata wafanyabiashara wakubwa wa dawa hizo wameingia woga na kiasi wanachoingia ni kidogo ambacho ni kati ya kilo nne hadi kilo tano.”Wengi wao wanaogopa kukamatwa.”
Kamishna wa Kitengo cha Kinga n
Kamishna wa Kitengo cha Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisiakitolea ufafanuzi katika baadhi ya mambo wakati wa mkutano huo kutoka kulia ni Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania TAFCA Bw. Simon Mwakifwamba na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Tanzania Joyce Fissoo
  • Pia amesema dawa za kulevya aina ya Heroin na Cocaini matumizi yamepungua na hivyo dawa ambazo zinatumika ni dawa za hospitali.
    Kuhusu kongamano la Februari 13 mwaka huu ,Kamishna Jeneral Sian’ga amsema lengo kuu ni kuhakikisha Watanzania wanaunganisha nguvu katika mapambano ya dawa za kulevya.
  • Hivyo kupitia kongamano hilo ambalo litawakutanisha wasanii mbalimbali nchini ambapo kupitia kongamano hilo itatolewa elimu inayohusu athari za matumizi ya dawa za kulevya, hivyo ametoa rai ya wasanii kujitokeza kwa wingi ili nao watoe maoni yao ya nini kifanyike kukomesha uingizwaji wa dawa za kulevya.
  • Wakati huo huo Kamishna wa Kitengo cha Kinga na Tiba wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Dk.Peter Mfisi amezungumzia umuhimu wa wasanii wa mashirikisho mbalimbali kushiriki kongamano hilo hasa kwa kuzingatia kuna baadhi ya wasanii wamekuwa wakitumia dawa za kulevya na wengine wanatumika kukubebeshwa dawa.
  • “Tatizo la dawa za kulevya ni la dunia nzima na wanaoatharika zaidi ni vijana wakiwamo wasanii maarufu ambao wengi wao wameathirika zaidi na wengine wamepoteza maisha kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya.
  • “Si kwamba wasanii hawajui kuwa dawa za kulevya zina athari,wanajua lakini wanaangalia leo lakini ukweli athari zake ni nyingi sana.Kwa bahati mbaya wanaotumia athari zake ni kubwa. Wapo wasanii ambao wametumika kubeba dawa za kulevya kutokana na ahadi za fedha badala ya kuelezwa na matatizo yanayopatikana kupitia dawa hizo. Hivyo kupitia kongamano hilo wataeleza athari zake,” amesema Dk.Mfisi.
  • Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini Tanzania Joyce Fissoo ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha wasanii wa mashirikisho mbalimbali kushiriki kongamano hilo huku akifafanua kundi ambalo linaathirika na utumiaji wa dawa za kulevya ni la wasanii.
  • “Tunaamini kuwa kupitia kongamano hilo ambalo mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ,wasanii watapa fursa ya kupata elimu inayohusu athari za dawa za kulevya.Tunaomba wasanii wote wajitokeze kwa wingi na wale wa mikoani tanaomba wafuatilie kongamano hilo kupitia vyombo vya habari,”amesema Fissoo.
  • Kamishna Jeneral wa mamlaka hiyo ataka watanzania kuunganisha nguvu ,aitaja MsumbujiPia azungumzia kongamano la wasanii ambalo mgeni rasmi atakuwa Mama Samia
Ad

Unaweza kuangalia pia

ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI – DKT. CHAULA

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *