Serikali imepunguza tozo ya ushuru ya mchuzi wa zabibu kutoka 3,315 hadi 450 kwa lita kwa kinywaji kikali kitokanacho na mchuzi wa zabibu.
Akichangia Bungeni katika Muswada wa Marekebisho ya Sheria Na.2/2019 Mbunge wa Viti Maalum Mh Mariam Ditopile ameishukuru serikali kwa kuleta mabadiliko hayo ya ushuru wa bidhaa na kupunguza tozo hiyo ambayo itawasaidia wakulima kupata soko la uhakika wa zabibu zao.
Aidh Mh Ditopile amatumia fursa hiyo kumpongeza Spika wa Bunge Mh Job Ndugai kwa kulisimamia suala hili kuelezea changamoto kubwa wanayoipata wakulima mkoani Dodoma,vile vile amempongeza Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde ambaye aliliwasilisha ombi kwa Mh Rais tarehe 23.04.2018 wakati wa ufunguzi wa Jengo la PSPF.
Kwa nyakati tofauti Mh Rais Magufuli alitoa maelekezo ya kuzitaka Wizara husika kulifanyia kazi suala hili kwa manufaa ya wakulima wa zabibu wa mkoa wa Dodoma.
Bunge la Jamhuri ya Tanzania limepitishwa muswada wa marekebisho ya Sheria ambao umelenga,pamoja na mambo mengine,kupunguza tozo ya Vinywaji vikali vitokanavyo na mchuzi wa Zabibu.
You have observed very interesting details! ps nice internet site.Blog money