Wafanyabiashara hao wakiendelea kupata ufafanuizi wa masuala mbalimbali

WAFANYABIASHARA MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WAONESHA NIA YA KUITUMIA BANDARI YA TANGA

  • Wafanyabiashara wa Mikoa ya kanda ya Kaskazini wameonesha nia ya kuanza kutumia Bandari ya Tanga kupitisha shehena ya mizigo yao baada ya kuridhishwa na mabadiliko makubwa ya mfumo wa utendaji wa Bandari hiyo.
Sehemu ya wafanyabishara
Sehemu ya wafanyabishara wakifuatilia mkutano huo katikati ni Meneja wa Bohari ya Mafuta ya GBP mkoani Tanga Amour
  • Wameonesha nia hiyo kwenye mkutano wa siku moja baina ya Uongozi wa mamlaka hiyo na wafanyabiashara hao na wadau mbalimbali kutoka mikoa ya Tanga,Kilimanjaro na Arusha.
Mwenyekiti wa TCCIA
Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Kilimanjaro Patrick Shirima akizungumza katika hafla hiyo
  • Katika mkutano huo wafanyabiashara hao waliongozwa na viongozi wa vyama vya Chemba za Biashara,Kilimo na Viwanda(TCCIA),Katibu tawala Msaidizi wao wa Kilimanjaro na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari nchini na uongozi wa mamlaka ya Bandari Tanga.
  • Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama amefafanua kuwa katika kuhakikisha bandari hiyo inatoa huduma bora kwa wateja wake imeboresha miundombinu na mifumo ya utendaji na ulinzi katika bandari hiyo.
KATIBU TAWALA
Katibu Tawala Msaidizi wa mkoa wa Kilimanjaro akizungumza kulia ni Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama
  • Amesema kuwa kutokana na maboresho hayo taratibu za uchukuaji wa mizigo zinatumia muda mchache tofauti na awali kutokana mamlaka zote za serikali zinazohusika na Bandari zipo kwenye jengo moja.
  • ” Tunataka kuwaondoa hofu wafanyabiashara kuwa sasa hivi Bandari ya Tanga ni nzuri,salama kwa mizigo na ni ya uhakika kutokana tumeboresha kuanzia mifumo ya ulinzi,miundombinu,utendaji kazi na Tehama” alisema.
Meneja wa Bandari
Meneja wa Bandari ya Tanga Percival Salama akizungumza na wafanyabiashara hao
  • Alieongeza ” Kutokana na maboresho hayo ikiwa mteja atakamilisha taratibu zote za uchukuaji wa mizigo basi kuanzia mizigo kufika bandarini atatumia siku tatu tu” alisema.
  • Katika kusogeza huduma zake kwa wateja wa mikoa ya Kaskazini ya Kilimanjaro na Arusha tayari uongozi wa mkoa wa Arusha kupitia mkuu wa mkoa huo Mrisho Gambo ametoa eneo lenye ukubwa wa ekari 500 eneo la Malula katika wilaya ya Arumeru kwa ajili ya ujenzi wa bandari kavu.
Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa Bandari
Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa Bandari nchini Lydia Mallya akizungumza ambapo aliwataka wafanyabiashara hao kutumia bandari hiyo kwani tayari ni bandari ya viwango vya kimataifa.
  • ” Wafanyabiashara wa Arusha na Kilimanjaro mtakuwa hamna haja ya kuja hadi Tanga kuchukua mizigo mtakuwa mnasubiri mizigo yenu huko huko Arusha sisi tunamiambia gharama zetu tu mnalipia moja kwa moja na sisi tutajuana na Shirika la Reli( TRC) ambao tunategemea ukarabati wa reli ukikamilika uwatumie wao” alisema.
  • Mwakilishi wa Mkurugenzi mkuu wa Bandari nchini Lydia Mallya aliwasihi wafanyabiashara hao kutumia bandari hiyo kwani tayari ni bandari ya viwango vya kimataifa.
  • Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Kilimanjaro Patrick Shirima amesema kuwa waliikimbia Bandari ya Tanga na kuhamia Bandari ya Mombasa nchini Kenya kutokana na urasimu uliokuwa unafanywa na taasisi za serikali zilizokuwa zinahusika na utoaji wa mizigo jambo ambalo lilikuwa linachelewesha mizigo.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SERIKALI INATARAJIA KUJENGA MINARA 5 YA MAWASILIANO WILAYANI MAFIA

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Injinia Atashasta Nditiye (Mb.) amezindua mnara wa Mawasiliano …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *