GAIRO SASA KUPATA MAJI SAFI NA SALAMA MWISHONI MWA MWEZI WA 3 2019

  • Mkuu wa Wilaya ya Gairo Siriel Mchembe, amewahakikishia wananchi wa Gairo kuondokana na tatizo la ukosefu wa maji safi na salama baada ya kukamilika kwa mtambo wa kuchuja chumvi.
MTAMBO WA KUCHUJA CHUMVI KWENYE MAJI
Mtambo wa kuchuja chumvi kwenye maji
  • Mkuu wa Wilaya amesema kuwa mtambo huo ambao unatengenezwa nchini Italy unatarajiwa kukamilika mwezi machi 2019.
  • Kwa upande wao Wenyeviti wa Serikali – Vitongoji vyote vya Mamlaka ya Mji Mdogo Wilayani Gairo,wamemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa kutoa hela kiasi cha shilingi bilion 2 kwa ajili ya mradi wa maji wilayani humo.
  • Mtambo huo utakaogharimu Bilioni 2 pesa za Kitanzania utasaidia kuondoa tatizo la maji katika Wilaya hiyo na wananchi wamemuomba mkuu wa Wilaya Mchembe, kuhakikisha Mamlaka ya maji ya Mkoa wa Morogoro(MORUWASA) kuanza kuhakiki mambomba na miundo mbinu ya mradi huo.
  • Mhe. Mchembe aliwaomba Wenyeviti wote wa Vitongoji kuhakikisha wanapitia maeneo ya kuunganisha maji kwenye mitaa yao ili kuhakikisha kama kuna changamoto zinafanyiwa kazi mapema.

Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI HASUNGA ASISITIZA ULAZIMA WA KUWA NA VIWANDA VYA MBOLEA NCHINI

Serikali imesema kuwa inathamini sana mchango wa Sekta binafsi katika kukuza uchumi kwani ndio chanzo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *