Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Iramba Mhe. Mwigulu Nchemba (kulia) mara baada ya kuwasili katika kiwanda cha kusindika alizeti cha Yaza katika kijiji cha Ndago, wilayani Iramba mkoa wa Singida.

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA WILAYANI IRAMBA MKOANI SINGIDA

  • Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameendelea na ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za maendeleo na amefanya ziara katika wilaya ya Iramba mkoani Singida.
  • Katika Wilaya ya Iramba Makamu wa Rais alitembelea kiwanda cha muwekezaji mzawa cha kusindika alizeti cha Yaza klichopo Ndago, pia alitembelea kituo cha afya cha Kinampanda na kujionea maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho pamoja na maboresho na ukarabati uliofanywa kwenye chuo cha Ualimu Kinampanda.
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mbunge wa Jimbo la Iramba Mhe. Mwigulu Nchemba (kushoto) mara baada ya kutembelea kiwanda cha kusindika alizeti cha Yaza katika kijiji cha Ndago, wilayani Iramba mkoa wa Singida.
  • Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ndago, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewapongeza wananchi wa tarafa ya Ndago kwa kuwa mstari wa mbele katika kushiriki kwenye shughuli za maendeleo.
    “Serikali inakuja na mpango ama sheria ya Bima ya Afya ambapo kila mmoja atatakiwa kuwa na bima ya afya” alisema Makamu wa Rais.
  • Makamu wa Rais amewakumbusha wakazi wa Iramba kukumbushana juu ya ugonjwa wa ukimwi kwani kasi ya maambukizi yameongezeka hivyo kila mtu ajichunge mwenyewe na wazazi wachunge watoto kwani maambukizo yanaanzia vijana wenye miaka 15 mpaka 24.
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia mara baada ya kutembelea kiwanda cha kusindika alizeti cha Yaza katika kijiji cha Ndago, wilayani Iramba mkoa wa Singida.
  • Kuhusu uwezeshaji vijana, wanawake na walemavu, Makamu wa Rais amezitaka Halmashauri kutenga asilimia 10% kama matakwa ya kisheria yanavyosema.
  • Pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais amewataka wananchi kuchagua viongozi wa serikali za mitaa na vitongoji wenye sifa.
  • “Sio tu kuhakikisha vitongoji na mitaa yote imerudi CCM ila kuchagua viongozi ambao wataendana na ajenda  ya maendeleo ya Serikali ya awamu ya tano”
SINGI-11
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo Cha Ualimu Bw. Maulid Njau (kushoto) juu ya maboresho na ukarabati wa chuo cha ualimu Kinampanda, wilayani Iramba mkoa wa Singida.
  • Kwa upande mwingine naibu Waziri Ujenzi Mhe. Elias Kuandikwa amewataka wanafunzi wa kijiji cha Ndago kuweka mkazo katika masomo ya Sayansi kwani nchi yetu inaelekea kwenye uchumi wa kati ambapo viwanda vitakuwa vingi na vitahitaji wataalamu kwa wingi.
  • Wakati huohuo Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko amesema kuwa hiki ni kipindi pekee cha Watanzania kufaidika na madini yao haswa baada ya kufanyika madadiliko mbali mbali.
MAKAMU W RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Chuo Cha Ualimu Bw. Maulid Njau (kushoto) juu ya maboresho na ukarabati wa chuo cha ualimu Kinampanda, wilayani Iramba mkoa wa Singida.
  • “leseni 40 zisizofanya kazi hapa na kupewa wachimbaji wadogo wadogo “.Alisema Waziri wa Madini. Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Iramba Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba ameishukuru Serikali ya awamu ya tano kwa niaba ya wananchi wa jimbo lake ambapo Serikali imetoa shilingi milioni 400 katika tarafa ya ndago kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya pamoja na gari ya wagonjwa.
  • Aidha Mbunge huyo amesema katika tarafa ya Ndago vijiji vinne ndani ya tarafa hiyo vimepata maji na wamejenga mabweni katika kila kata.
Ad

Unaweza kuangalia pia

LIVE: UZINDUZI WA MAJENGO YA OFISI YA MANISPAA NA MKUU WA WILAYA KIGAMBONI JIJINI DSM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *