- Mheshimiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ameanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Tabora ambapo atatembelea Wilaya zote saba (7) za Igunga, Nzega, Uyui, Sikonge, Kaliua, Urambo na Tabora .
- Lengo la ziara ni kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ili kujionea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015 ya Chama Cha Mapinduzi, kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo na kutoa maelekezo kwa watendaji kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji yatakayobainika katika ziara.
Ad