- Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan leo ameanza ziara ya kikazi katika Mkoa wa Tabora ambapo atatembelea Wilaya zote saba (7) za Igunga, Nzega, Uyui, Sikonge, Kaliua, Urambo na Tabora.
- Akiwa wilayani Igunga Makamu wa Rais alipokea taarifa ya utekelezaji ya mkoa liyosomwa na Mkuu wa mkoa huo Mhe. Aggrey Mwanri katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, na kukagua maendeleo ya ujenzi wa tanki kubwa la maji ikiwa sehemu ya utekelezaji wa mradi wa maji wa shilingi bilioni 600 ambao utekelezaji wake umefikia asilimia 58% kisha kutembelea maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya Simbo ambapo alipanda mti wa kumbukumbu na kuhutubia wananchi wa Simbo.
- Ziara za Makamu wa Rais zina lengo la kuhamasisha na kukagua shughuli za maendeleo kama ilivyoahidiwa kwenye ilani ya uchaguzi ya 2015.
- Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Simbo katika jimbo la Manonga wilayani Igunga Makamu wa Rais aliwaambia wananchi hao kuwa tatizo kubwa la wilaya ya Igunga ni ukosefu wa vyanzo vya maji.
- “Serikali itafanya kila linalowezekana kuhakikisha maji ya kutosha yanapatikana Igunga”alisema Makamu wa Rais.
- Katika suala la afya wilaya ya Igunga ina Vituo 66 vya afya kati ya hivyo 55 vinamilikiwa na Serikali.
- Makamu wa Rais amehimiza Elimu ya kutosha kwa wananchi juu ya umuhimu wa bima ya afya ambapo Serikali inajiandaa na mpango wa Bima kwa wote.
- Makamu wa Rais pia amewataka Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kutoa elimu ya kutosha kwa wafanya biashara wadogo wadogo na kuhakikisha wale wenye sifa ndio wanapata vitambulisho.
- Katika ziara yake mkoani Tabora Makamu wa Rais ameambatana na Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko, Naibu Waziri Maji Mhe. Juma Aweso, Naibu Waziri Ujenzi Mhe. Elias Kwandikwa na Naibu Waziri TAMISEMI Mhe. Mwita Waitara .
Ad
I was looking at some of your content on this site
and I conceive this site is really informative! Keep posting.!
I blog quite often and I really appreciate your information. The article has really peaked my interest. I will take a note of your site and keep checking for new information about once per week. I opted in for your RSS feed as well.
Very nice article. I certainly love this site. Keep writing!