Imefanyika usiku wa siku ya wapendanao (valentine’s day)
Iliandaliwa jijini Mbeya
Ilihusisha viongozi mbali mbali, wakazi wa mkoa wa Mbeya, mikoa jirani sambamba na wapendanao walioongozwa na Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Dkt. Tulia Akson
Waliafikiana kuisaidia ujenzi wa nyumba, malazi, kuwaonyesha upendo familia ya Timotheo na mkewe Salome ambaye ni mwenye ulemavu na ana mtoto mdogo wa miezi kadhaa.
Ni valentine pekee iliyogusa wengi waliohudhuria na kushiriki kuwasaidia wanandoa hao ambao walialikwa kama wageni maalum.
Wote waliohudhuria waafikiana kuendeleza aina hiyo ya usheherekeaji wa siku ya wapendanao na kuwasihi Watanzania wengine kuiga.
Fuatilia video hii kushuhudia wageni hao maalum walivyoonyeshwa upendo wa kweli siku hiyo