- Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa sita wa Baraza la Mawaziri wa Maji wa nchi nane la watumiaji wa maji wa mto Zambezi utakao fanyika mnamo Februari 28 mwaka huu jijini Dar Es Salaam.
- Hayo yamesemwa na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbarara wakati akiongea katika kikao cha waandishi wa habari kilichofanyika mkoani Tanga.
- Amesema kuwa Tanzania ni mmoja wa wanachama washiriki wa usimamizi wa maji katika mabonde saba kati ya mabonde tisa yaliyopo katika ukanda wa mto Zambezi.Hivyo alisema kuwa mkutano huo utatanguliwa na mkutano wa saba wa wataalamu wa maji ambao utafanyika mnamo februari 26 na 27 mwaka huu jijini Dar Es salaama.
- Amesema kuwa mkutano huo unalenga katika kuweka mikakati ya namna ya kusimamia raslimali za maji pamoja na kutunza mazingira ya vyanzo vya maji kwa maendeleo endelevu ya nchi wanachama wa umoja huo.
- “Takwimu zinaonyesha Tanzania kupitia bonde la ziwa Nyasa inachangia karibu asilimia 11.3% ya maji yote yaliyoko katika Mto Zambezi huku nchi nyingine zikichangia kwa kiwango kilichobaki”alisema Waziri Mbarawa.
- Pia alisema kuwa katika mkutano huo Mawaziri hao wataweza kupata fursa ya kujadili na kupitisha mpango mkakati wa matumizi ya maji ya mto Zambezi ukihusisha miradi mbalimbali ya sekta hiyo.
- “Tutaweza kujadili kwa pamoja taarifa ya hali ya mazingira ya bonge hilo pamoja na kupitisha mwongozo wa namna ya kubadilishana takwimu za raslimali za maji”alisema Waziri huyo. Mawaziri wa nchi za Angola ,Botiswana,Zambia ,Zimbabwe,Botswana ,Msumbiji,Malawi,Namibia,na mwenyeji Tanzania wanatarajiwa kushiriki katika mkutano huo
Ad