Jengo la Uwanja wa Ndege cha Julius Nyerere Teminal Three jijini Dar es salaam ambalo Februari 28, 2019, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alikagua ujenzi wake na kuambiwa kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na linatarajiwa kuwa limekamilika Mei mwaka huu.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kusema ameridhishwa hatua iliyofikiwa.
Mradi wa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 95 na unatarajiwa kukamilika Mei 30, mwaka huu ambapo hadi sasa tayari maeneo mengi yamekamilika ikiwa ni pamoja na sehemu za abiria wanaowasili na kuondoka.
Waziri Mkuu ambaye ametembelea mradi huo (Alhamisi, Februari 28, 2019) amesema amefurahi kukuta michoro ya wanyama kama tembo, twiga, bahari, minazi na majahazi ambayo ni alama za nchi.
Kufuatia kukamilika kwa uwanja huo kwa asilimia 95, Waziri Mkuu ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) ianze kukamilisha taratibu za kuutumia uwanja huo ili mkandarasi anapoukabidhi uanze kutumika.
Kadhalika, Waziri Mkuu ameipongeza kampuni inayojenga uwanja huo kwa kazi nzuri waliyoifanya kwa sababu jengo ni zuri na linavutia. Pia amewapongeza Watanzania wanaofanya kazi kwenye mradi huo.
Awali, akisoma taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi wa Walaka wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale alimuelezwa Waziri Mkuu kuwa jengo hilo umekamilika kwa asilimia 95.05, ambapo eneo la maegesho ya ndege linaweza kuegesha ndege 19 za darala C, na 11 daraja E na jengo linaweza kuhudumia abiria 2,800 kwa saa muda ambao abiria ni wengi.
Mhandisi Mfugale amemhakikishia Mhe,. Majaliwa kuwa ujenzi huo utakamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyowekwa, na kwamba jengo hilo litakabidhiwa kwa serikali tarehe 31 Mei, 2019.