SERIKALI YAPATIWA MKOPO WA SH. BILIONI 589.26 KUTOKA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AfDB)

KATIBU MKUU
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akibadilishana mkataba na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) hapa nchini Dkt. Alex Mubiru mara baada ya kutiliana saini mikataba miwili ya mkopo wa masharti nafuu wa kiasi cha Shilingi bilioni 589.26 itakayotumika katika ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Kabingo(Kakonko)-Kasulu-Manyovu km 260 mkoani Kigoma.
KATIBU  MKUU
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza jambo kuhusiana na ramani ya ujenzi wa barabara ya kutoka Kabingo(Kakonko)-Kasulu-Manyovu km 260 zitakazojengwa kwa kiwango cha lami mkoani Kigoma.
KATIBU MKUU
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza jambo na wanahabari kuhusiana na mkopo huo wa masharti nafuu ambao utatumika katika ujenzi wa barabara mkoani Kigoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya (Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga.
KATIBU MKUU
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James kulia akisaini mkataba wa Mkopo wa Masharti nafuu wenye thamani ya Shilingi bilioni 589.26 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB iliyowakilishwa na Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo hapa nchini Dkt. Alex Mubiru (kushoto akisaini) katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam. Fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Kabingo(Kakonko)-Kasulu-Manyovu km 260 mkoani Kigoma.
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI KAMWELWE AZINDUA BODI MPYA YA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amezindua Bodi mpya ya Shirika la …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *