- Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora(UYUI) umeagizwa kuongeza kasi katika ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ili ifikapo Juni mwishoni mwaka huu majengo yote waliyopangiwa yamewe yamekamilika.
- Agizo hilo limetolewa wilayani Uyui na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi huo.
- Alisema fedha zipo hakuna sababu ya kazi ya ujenzi kwenda pole pole kwa kuwa wananchi wanasubiri huduma hiyo kwa hamu.
- Jafo alisema katika Halmashauri nyingine ambapo walipewa fedha pamoja tayari majengo yao yako usawa wa madirisha lakini ya Uyui bado yako katika ngazi za msingi.
- Alisema sio vizuri kutumia fundi mmoja kujenga majengo yote ni vema wakatumia mafundi wengi ili kuharakisha kazi ya ujenzi wa Hospitali hiyo.
- Aidha Waziri huyo alisema ni jambo la kusikitishwa kuona Halmashauri hiyo imetumia kiasi cha milioni 8 kusafisha eneo badala ya kuwahamisha wananchi kushiriki katika usafishaji wa ili fedha hizo zisaidie ujenzi.
- Alisema fedha walizozitumia katika usafishaji wa eneo zingeweza kusaidia katika uendeleza wa ujenzi wa majengo hayo kama wananchi wangeshiriki katika usafishaji wa eneo badala ya kukodi Greda na kulipa kiasi hicho cha fedha.
- Naye Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya alimwakikishia Waziri kuwa watajitahidi kukamilisha majengo hayo katika kipindi kilichopangwa na kwa kuzingatia maelekezo ya TAMISEMI ili fedha zitakazobaki zisaidie kujenga kichoma taka.
Ad