TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA KIMATAIFA WA WARATIBU WA MIRADI YA ATOMIKI

  • Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojiaa  Profesa Joyce Ndalichako  anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa kimataifa wa waratibu wa kitaifa wa miradi inayotekelezwa na Shirika la nguvu za Atomiki duniani kwa nchi  46 kanda ya Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe 11 hadi 15 mezi Machi  jijini Arusha wenye lengo la kujadiliana na masuala mbali mbali.
  • Mkutano huo utashirikisha washiriki 60 kutoka nchini 46 duniani kutoka bara la Afrika ambao ni wanachama wa Shirika la nguvu za Atomiki duniani ambao wataweza kujadiliana  masuala mbali mbali .
  • Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania ,Profesa Lazaro Busagala amaesema maandalizi ya mkutano huo yamekamilika na kwamba wana imani mkutano huo utaweza kusaidia nchi washiriki kuweza kusonga mbele katika namna ya uboreshaji wa sekta mbali mbali kutokana na miradi inayofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki Duniani(IAEA).
  • Amesema katika mkutano huo ,washiriki watapata nafasi ya kujadiliana kwa mapana juu ya namna ya.
  • Pia Profesa Busagala ameongeza kuwa mkutano huo pia utahudhuriwa na  Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa  la Nguvu za Atomiki kanda ya AFrika Bwana  Shaukat Abdrazak ambaye baada ya mkutano huo ataweza kufanya mazungumzo na viongozi mbali mbali na uongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Wizara nne ambazo zimekuwa zikihusika katika miradi mbali mbali ya kitaifa inayotekelezwa na Shirika la Nguvu za Atomiki duninia(IAEA) .
  •  Kwa upande wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ,Mkurugenzi Shaukat atakutana na Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi .
  • Kwa upande wa Tanzania Bara Shaukat atafanya mazungumzo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano  wa Afrika Mashariki,Waziri wa Maji .
  • Pia ataweza kufanya ziara katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Seliani,Taasisi ya Chakula na Lishe na Taasisi ya Saratani Ocean Road.
  • Profesa Busagala amesema kuwa mazungumo hayo yataweza kusaidia nchi kwenye uboreshaji wa miradi mbali mbali inayofanyika hapa nchini hasa katika sekta ya Afya,Kilimo,maji.
  • Ameeeleza kuwa Tanzania ni moja ya nchi iiliyoweza kufadika kwa kiasi kikubwa kwa miradi  katika ya udhibiti na kuhamasisha  matumizi salama  ya tekenolojia  ya nyuklia  inayotekelezwa na Shirika la Nguvu za Atomiki duniani .
Ad

Unaweza kuangalia pia

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA MKUTANO WA WOMENLIFT HEALTH

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Maelezo kutoka kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *