Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya ndege ya Air Tanzania aina ya Airbus A220-300 wakati akielekea nchini Uganda kuhudhuria mkutano wa Africa Now Summit 2019 unaoanza kesho tarehe 12 mjini Kampala Uganda.

MAKAMU WA RAIS AWASILI NCHINI UGANDA TAYARI KWA KUSHIRIKI MKUTANO WA AFRICA NOW SUMMIT 2019

MAKAMU WA RAIS

  • Makamu wa Rais  Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Uganda na kupokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mhe. Philemon Mateke pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Dkt. Aziz P. Mlima katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Entebe.
  • Makamu wa Rais pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaru wamesafiri na ndege ya abiria ya Shirika la Ndege  la Tanzania aina ya Airbus A220-300 (Dodoma) kutoka jijini Dar es Salaam mpaka Entebe kupitia Kilimanjaro.

MAKAMU WA RAIS

  • Tarehe 12 machi 2019, Makamu wa Rais atashiriki mkutano wa mwaka 2019 wa “Africa Now Summit 2019” ambao utafunguliwa na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ambapo viongozi mbalimbali wa Afrika wanakutana ili kupata majibu ya changamoto za Afrika katika masuala ya kiuchumi.
  • Katika mkutano huo wa Viongozi wa Afrika, Makamu wa Rais anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambapo katika mada mbalimbali zitakazojadiliwa Makamu wa Rais atazungumzia suala la Uongozi unaohitajika kuchochea mabadiliko ya Kijamii na Uchumi Afrika.

SAMI-3

  • Viongozi wengine watakaotoa mada ni Rais wa Misri ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (UA) Mhe. Abdel Fattah el Sisi; Rais wa Afrika Kusini Mhe. Cyril Ramaphosa; Makamu wa Rais wa Kenya Mhe. William Ruto; na Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Ahmed Abiy na Rais Paul Kagame wa Rwanda. Mada zote hizi zitajikita kwenye kuonesha chachu ya Uongozi katika kuleta maendeleo endelevu barani Afrika.
  • Mkutano utamalizika tarehe 13 Machi 2019 utaanza na hotuba kutoka kwa Rais wa Somalia Mhe. Mohamed Abdullahi na baadae kufungwa rasmi na mwenyeji wake Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.
  • Makamu wa Rais ataambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro.
Ad

Unaweza kuangalia pia

TANZANIA YATAKA AMANI KUPUNGUZA MZIGO WA WAKIMBIZI AFRIKA

Tanzania imetaka Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada na nguvu katika kuleta …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *