WAZIRI BITEKO ATETA NA WENYE NIA YA KUWEKEZA NCHINI

MADINI-2
Waziri wa Madini Doto Biteko akizungumza jambo na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer. Anayefuatilia ni Mkurugenzi wa Ssera na Mipango Wizara ya Madini, Augustine Ollal.
  • Waziri wa Madini Doto Biteko amekutana na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer ambaye amemweleza Waziri Biteko kuhusu ujio wa kampuni zipatazo 3 kutoka mataifa mbalimbali zenye nia ya kuwekeza katika sekta ya madini.
  • Dkt. Gollmer amesema kampuni hizo zimeonesha nia ya kuwekeza katika sekta ya madini hususan katika masuala ya utafiti na uchimbaji wa madini kutokana na ushawishi unaofanywa na Balozi wa Tanzania nchini Urusi Meja Jenerali Mstaafu Simon Mumwi  ambaye amekuwa akihamasisha watu wa mataifa mbalimbali nchini humo kuwekeza nchini.
WAZIRI WA MADINI
Waziri wa Madini Doto Biteko akiteta jambo na Rais wa Kampuni ya Amtec Resources Management Ltd ya nchini Uingereza, Dkt. Peter Gollmer. Kulia wanaofuatilia ni Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa na Katibu wa Waziri, Kungulu Kasongi.
  • Pia, ameeleza kwamba, kampuni hizo hazina shaka ya kuwekeza Tanzania kutokana na mazingira tulivu ya kisisasa yaliyopo nchini pamoja na utajiri wa rasilimali madini ambayo Tanzania imejaliwa kuwa nayo.
  • Akizungumza katika kikao hicho, Waziri Biteko amemweleza Dkt. Gollmer kuwa kikao hicho ni muhimu na kwamba milango kwa ajili ya wawekezaji wenye dhamira ya dhati ya kuwekeza nchini iko wazi na kuongeza kuwa, kama wizara inaratajia kukutana na kampuni hizo.
  • Wengine walioshiriki kikao hicho ni Kamishna wa Madini Mhandisi David Mulabwa, Mkurugeni wa Idara ya Sera na Mipango, Augustine Ollal na Katibu wa Waziri Kungulu Kasongi.
Ad

Unaweza kuangalia pia

MADINI NA VIWANDA VYALETA MAGEUZI YA UCHUMI NCHINI

Mauzo ya bidhaa nje ya nchi zisizo kuwa za kawaida yameongezeka kwa asilimia 41.9 kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *