MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA WATANZANIA WANAOISHI UGANDA

  • Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Magufuli pamoja na wasaidizi wake imeamua kufanya kazi kwa bidii sana kukuza uchumi wake.
  • Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati alipokutana na Viongozi wa Watanzania wanaoishi nchini Uganda katika hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort jijini Kampala.
  • Katika kuleta uchumi wa viwanda Serikali imedhamiria kuongeza na kuboresha upatikanaji wa Umeme, huduma ya maji, kuboresha mitaala ya elimu,kuboresha huduma za afya pamoja na miundombinu.
MAKAMU WA RAIS
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa Africa Now Summit 2019 katika hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort mjini Kampala, Uganda.
  • Makamu wa Rais amewaambia Viongozi hao wa Watanzania wanaoishi Uganda kuwa miradi mingi inayofanyika Tanzania inafanyika kwa kutumia fedha za ndani.
  • Pamoja na mambo mengine Makamu wa Rais amewataka Watanzania waishio nje ya Tanzania kuja kuwekeza nchini kwani kuna maboresho mengi ya kuvutia wawekezaji yamefanyika.
  • Kwa upande mwingine Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema kuna Watanzania zaidi ya milioni 2 wanaishi nchi za nje hivyo amewaomba kuwa mabalozi wazuri wa kuisemea nchi yao.
  • Kuhitimisha mkutano wa Africa Now Summit 2019, Makamu wa Rais alipata nafasi ya kuchangia katika suala zima la mtazamo wa kijinsia ambapo alisema bado wanawake hawapewi nafasi ya kutosha kwenye mambo mengi ya msingi kuanzia kwenye elimu, uongozi na masuala mengine ya huduma za kijamii katika hili Makamu wa Rais alizungumzia suala zima la wanawake wanaofanya biashara za mipakani wamekuwa wakinyanyasika na kuna wakati wanaonekana ni watu wa kupitisha magendo hivyo kushauri mamlaka husika kutambua na kusaidia wanawake hawa ambao wanachokitafuta ni cha kuhudumia familia ama jamii nzima.
  • Mwisho Makamu wa Rais alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, Kampala Uganda.

Ad

Unaweza kuangalia pia

TANZANIA YATAKA AMANI KUPUNGUZA MZIGO WA WAKIMBIZI AFRIKA

Tanzania imetaka Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada na nguvu katika kuleta …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *