Miradi ya Kimkakati ya kuongeza mapato katika Halmashauri:
- Hatua iliyofikiwa ni utekelezaji wa miradi ya kimkakati 37 ya kuongeza mapato ya halmashauri na kupunguza utegemezi wa kibajeti kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali ikijumuisha Soko la kisasa – manispaa ya Morogoro, soko la kisasa – halmashauri ya mji Kibaha, Pwani, ghala la kisasa – halmshauri ya wilaya ya Ruangwa, kituo cha mabasi Mbezi Louis – Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, soko la Mburahati – manispaa ya Ubungo, Dar es Salaam, ujenzi na upanuzi wa kiwanda cha kutengeneza chaki na kiwanda cha vifungashio – halmashauri ya wilaya ya Maswa, Simiyu, stendi ya mabasi Korogwe. Miradi hii inatekelezwa katika halmashauri 29 na ipo katika hatua mbalimbali.
Ad