Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Bi. Hodan Addou, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wanawake (UN-Women), pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Bw. Alvaro Rodriguez (katikati) ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.
MAKAMU WA RAISA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAZI WA UN WOMEN
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Wanawake (UN-Women) Bi. Hodan Addou aliyeambatana na Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa Bw. Alvaro Rodriguez, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine Mwakilishi huyo wa UN-Women alizungumzia kazi mbalimbali zinazofanywa na Shirika hilo hapa nchini hususani katika kushirikiana na Serikali katika miradi mbalimbali ikiwemo Mkakati wa Kukuza Uchumi na kupumguza Umasikini Tanzania(MKUKUTA) na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Zanzibar (MKUZA).