- Ikiwa ni muendelezo wa majadiliano mbalimbali kuhusu mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania (EACOP), Kamati za Ulinzi na Usalama za mradi kutoka nchi hizo zimekutana jijini Kampala kwa lengo kujadili masuala ya usalama ya mradi huo.
- Kikao kati ya pande hizo mbili kilianza tarehe 18/3/2019 na kuhitimishwa tarehe 20 mwezi huu na Wawakilishi wa Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa nchi hizo mbili ambapo kuliandaliwa Makubaliano ya Awali (MoU) ya ulinzi na usalama ya mradi wa Bomba la Mafuta.
- Makubaliano ya Awali (MoU) ya ulinzi na usalama ya mradi huo yanatarajiwa kusainiwa katika vikao vijavyo vya ngazi ya Mawaziri wa nchi husika.
Ad