- Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga amezindua kampeni ya usajili wa watoto chini ya miaka mitano na kuwapatia vyeti vya kuzaliwa kwa mikoa ya Dodoma na Singida.
- Akizindua kampeni hiyo, Dkt. Mahiga ameitaka RITA kuhakikisha inatunza taarifa za watoto wanazozichukua kupitia mtandao wa simu na kuhakikisha zinapatikana pale zitakapohitajika.
- “Kuwasajili watoto hawa kwa kasi hii ni vizuri lakini kazi kubwa ni kuhakikisha taarifa hizo zinawekwa na kutunzwa kule zinakostahili na zinapatikana wakati wote”, alisema Dkt Mahiga.
- Amesema Serikali itaendelea kulinda haki za msingi za raia wake na ndio maana umeamua kutekeleza mpango wa Usajili na utoaji vyeti vya kuzaliwa kwa watoto chini ya miaka mitano kwa kuwa cheti cha kuzaliwa ni haki ya kila mtoto.
- Amesema cheti cha kuzaliwa ni alama na vitambulisho wa uraia wa kila mtu na kwamba Tanzania imeamua raia wake wote wawe na utambulisho wao.
- Akizungumza katika uzinduzi huo Mtendaji Mkuu wa RITA bibi Emmy Hudson amesema tangu kuanza kwa awamu ya kwanza ya kampeni hiyo jumla ya watoto milioni tatu wamesajiliwa na kupewa vyeti katika mikoa ya Mbeya, Mwanza, Simiyu, Geita, Njombe, Iringa, Songwe, Mara, Musoma, Lindi, Mtwara, Dodoma na Singida na inakadiriwa hadi kampeni hiyo itakapokamilika mwisho ni mwa mwezi huu zaidi ya watoto milioni tatu na nusu watakuwa wamesajiliwa.
- Awali akizungumza katika uzinduzi huo Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi aliahidi kukusimamia Mkoa wa Singida ili uweze kufanya usajili kwa watoto zaidi ya lengo lililorekebishwa la watoto 280,000 ndani ya wiki mbili ambapo alisema hadi kufikia Machi 20 mkoa wake ulikuwa umesajili zaidi ya watoto 180,000
- Kazi ya usajili wa watoto hao inafanywa na wasajili wasaidizi ambao wamepewa Mafunzo maalum ya kuingiza taarifa za watoto kwa kutumia simu ya Mkononi na inafanyika katika vituo vyote vya afya na katika ofisi za kata ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.
- Uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya stendi mjini Singida na kuhudhuriwa na viongozi na watendaji wa serikali kutoka mikoa ya Singida na Dodoma wadau wa maendeleo wa UNICEF, CANADA na kampuni ya TIGO ambayo imetoa simu na mtandao wa simu wake unaothmika kufanya usajili wa watoto katika mikoa hiyo nchini.
Ad
Казахский национальный технический университет https://satbayev.university им. К.Сатпаева
Sadio Mane https://al-nassr.sadio-mane-ar.com the Senegalese footballer best known for his performances at clubs such as Southampton and Liverpool, has become a prominent figure in Al Nassr.
Brazilian footballer Ricardo Escarson https://orlando-city.kaka-ar.com dos Santos Leite, better known as Kaka, is one of the most famous and successful players in football history.
Edson Arantes https://santos.pele-ar.com do Nascimento, known as Pele, was born on October 23, 1940 in Tres Coracoes, Minas Gerais, Brazil.
дизайн частных интерьеров https://dizayn-interera-doma.ru
The road to the Premier League https://english-championship.premier-league-ar.com begins long before a team gets promoted to the English Premier League for the first time
In recent years, the leading positions in the Spanish https://spanish-championship.laliga-ar.com championship have been firmly occupied by two major giants – Barcelona and Real Madrid.