Kituo cha afya cha Bwisya Ukara, Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza

UJENZI WA KITUO CHA AFYA BWISYA UKARA MKOANI MWANZA WAKAMILIKA

KITUO CHA AFYA
Kituo cha afya cha Bwisya Ukara, Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza
  • Majengo ya kituo cha afya cha Bwisya Ukara, Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza Kilichojengwa kwa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli yamewavutia na kuwafurahisha wananchi wa eneo hilo ambao walikuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya upatikanaji wa huduma za matibabu.
KITUO CHA AFYA
Kituo cha afya cha Bwisya Ukara, Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza
  • Kukosekana kwa huduma za kituo cha afya katika eneo hilo kulisababisha wananchi kulazimika kutumia mitumbwi na maboti kufuata huduma za matibabu mbali, hali iliyosababisha ajali za majini na vifo.
Screen Shot 2019-03-22 at 17.27.33
Muonekano wa ndani wa Kituo cha afya cha Bwisya Ukara, Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza
  • Rais Magufuli alitoa maagizo ya kujengwa kituo hicho Baada ya ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama katika ziwa Victoria Septemba 2018, Mhe. Rais Magufuli alielekeza fedha za michango iliyotolewa na watu mbalimbali, mashirika na taasisi kuelekezwa katika ujenzi wa kituo cha afya ili kutatua kero kubwa ya changamoto ya upatikanaji wa matibabu.
KITUO CHA AFYA
Kituo cha afya cha Bwisya Ukara, Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza
KITUO
Kituo cha afya cha Bwisya Ukara, Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza
  • Wananchi hao wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kuwasaidia kutatua tatizo hilo.
Ad

Unaweza kuangalia pia

ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI – DKT. CHAULA

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *