Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 26, Machi 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Ndugu Theobald Maingu Sabi ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi huyo amefika ofisini kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kujitambulisha akiwa ameongozana na Meneja mahusiano na Serikali Bw. William Kalaghe pamoja na Afisa Masoko wa NBC Bi. Neemarose Singo.
pamoja sana