TANZANIA IMEONGOZA KUVUTIA WAWEKEZAJI KATI YA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

UWEKEZAJI 

  • Sekta ya Uwekezaji imeendelea kukua ikilinganishwa na nchi nyingine za Afrika Mashariki ambapo ripoti mbalimbali za uwekezaji duniani zinaonesha Tanzania imeongoza kwa kuvutia uwekezaji kati ya nchi za Afrika Mashariki.
  • Kwa mfano, Ripoti ya Uwekezaji ya Dunia ya mwaka 2018 inayotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo (UNCTAD) inaonesha kuwa Tanzania imevutia uwekezaji wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 1,180, ikifuatiwa na Uganda Dola za Kimarekani milioni 700 na Kenya Dola za Kimarekani milioni 672.
  • Aidha, ripoti ya “Where to Invest in Africa” ya mwaka 2018 inayojulikana kama RMB’s Investment Attractiveness Index inayoonesha nchi zinazovutia zaidi kwa uwekezaji barani Afrika, Tanzania imeendelea kuwa katika kumi bora kwa kushika nafasi ya saba (7) kati ya nchi 52 ikipanda kutoka nafasi ya 9 mwaka 2017.
  • Aidha, jitihada za Serikali kuhamasisha ujenzi wa viwanda nchini zimewezesha kuongezeka mitaji katika viwanda mwaka hadi mwaka.
  • Kwa mfano, mtaji uliowekezwa chini ya Mamlaka ya EPZ umeongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 1.422 mwaka 2016 hadi Dola za Marekani bilioni 2.23 hapo Novemba, 2018, ikiwa ni ongezeko la Dola za Marekani milioni 808 (sawa na ongezeko la asilimia 56.8).
  • Mwenendo wa mauzo ya bidhaa za viwanda hivyo nje ya nchi yamekuwa yakiongezeka mwaka hadi mwaka na kufikia Dola za Marekani bilioni 2.194 hapo Novemba 2018, kutoka Dola za Marekani bilioni 1.1 mwaka 2016, ikiwa ni ongezeko la asilimia 99.45.
  • Mtaji mkubwa umewekezwa katika viwanda vya kuongeza thamani mazao (agro processing) ambapo ina asilimia 38 ya mtaji wote; zikifuatiwa na viwanda vya kuunganisha mitambo (assembling & engineering) asilimia 31 ya mtaji, mavazi na nguo asilimia 21 ya mtaji na uchakataji madini asilimia 10 ya mtaji.
  • Aidha, viwanda 71 ni vya makampuni ya kigeni, viwanda 58 ni vya makampuni ya ubia na viwanda 45 ni vya makampuni ya ndani.
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI KAIRUKI AWAHAKIKISHIA WAWEKEZAJI MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe. Angellah Kairuki …

Oni moja

  1. Tuongeze bidii zaidi katika uzalishaji na ukuaji wa viwanda vyetu ili tuweze kusimama zaidi.
    tunapenda kulewa sifa na kuanza kubweteka,mafanikio tuliyo fikia chini ya mikwara na misuli ya Mh.Rais wetu tusifanye tukarudi nyuma na kujilaumu.
    it can be done more effectively than now,lets work together and harder for the betterment of our country’s economy

Leave a Reply to PRIVANUS Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *