PROF PALAMAGAMBA AKUTANA NA BARONESS LYNDA CHALKER

  • Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi amesema mabadiliko yote ya sheria yaliyofanyika hivi karibuni katika sekta za madini,maliasili na uwekezaji yana lengo la kuweka mazingira bora zaidi yatakayoleta tija kwa Taifa na wawekezaji kutokana  na sheria mpya kuondoa utaifishaji (nationalization) na upokonyaji mali (confiscation).
  • Profesa Palamagamba John Kabudi ameyasema hayo wakati wa mazungumzo na Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited Mhe. Lynda Chalker na kuongeza kuwa hatua zilizochukuliwa na serikali ya awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli ni kuweka uwanda sawa kwa kuondoa rushwa na urasimu na kumtaka Mhe Chalker kuhamasisha wawekezaji kutoka Uingereza kuja kuwekeza hapa nchini.
  • Katika mazungumzo hayo Profesa Palamagamba John Kabudi amemuahakikishia Mwenyekiti huyo wa Taasisi ya  Africa Matters limited kuwa mazingira ya uwekezaji nchini ni salama na yameboreshwa zaidi na hakuna masuala ya utaifishaji (nationalisation) wala upokonyaji mali (confiscation) kama inavyopotoshwa na baadhi ya watu wasioitakia mema Tanzania.
  • “Katika kutekeleza diplomasia ya Uchumi Tanzania inatoa kipaumbele kwa uwekezaji wenye tija kwa Taifa na unaozingatia maslahi ya pande zote (Win – win situation) kwa kuwa sasa kupitia sheria mpya tuna mfumo wa kodi unaofahamika, misamaha ya kodi isiyo na upendeleo na si kweli kuwa mazingira yamebadilika na kusema kweli kilichbadilika ni usimamizi madhubuti,kupambana na rushwa na kuhakikisha kodi stahiki inalipwa”
  • Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Africa Matters Limited Mhe. Lynda Chalker amempongeza Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini na kuongeza kuwa atakaporejea Uingereza msafara wa wafanyabiashara na wawekezaji kuja Tanzania na kwamba kuna uwezekano mkubwa wa uwepo wa mabadiliko ya kisiasa nchini Uingereza na marafiki wa Jumuia ya madola kama Tanzania wanapewa kipaumbele katika uwekezaji na ujenzi wa viwanda.
  • “Ninadhani wawekezaji hasa wa nje ya Tanzania wanahitaji kufanya utafiti kidogo kuhusu kile Tanzania inachokihitaji na namna  watakavyonufaika kwa kuwekeza Tanzania,nimuahidi waziri hapa kuwa nitakaporejea London, nitakutana na mjumbe maalum wa Uingereza wa mambo ya biashara kwa Tanzania pia nitaonana na mawaziri wa mambo ya nje wa Uingereza na Jumuia ya Madola kuona  uwezekano wa kuwa na mkutano mkubwa ambao utazungumzia zaidi masuala ya uwekezaji na biashara kwa Tanzania”
Ad

Unaweza kuangalia pia

TANZANIA YATAKA AMANI KUPUNGUZA MZIGO WA WAKIMBIZI AFRIKA

Tanzania imetaka Umoja wa Afrika na Jumuiya za Kimataifa kuongeza jitihada na nguvu katika kuleta …

Oni moja

  1. Damian's J Mushi

    Prf Palamagamba amefanya vizuri sana kukutana na Linder chawlker na kuzungumzia habari za uwekezaji na Sheria zilizobadilishwa kwa ajili ya maslahi mazuri ya pande zote. Wawekezaji na serikali, na kumwomba atutafutie wawekezaji kutoka UK na kuwaeleza kwamba nia ya serikali na Sheria mpya za uwekezaji hasa kwenye madini haimaanishi kutaivisha au kufilisi Mali za wawekezaji Kama inavyo tangazwa na wale wasio itakia mema serikali yetu? Tunafurahi kwamba huyo mwakoshi ameahidi kwamba akirudi nyumbani atajaribu kukutana na waziri husika kumweleza hayo yote na kuangalia ni wapi wafanya biashara kutoka UK wanapoweza kuwekweza? Je amewahi kumkumbusha ya mwekezaji wetu acacia na kutokubaliana na serikali na hayo mabadiliko ya Sheria pamoja na ulipaji kodi ya uhalisia kwa serikali??tunatemea kamwambia na anaweza kusaidia sana Kama alivyo saidia kwenye Ile Rada na tukupewa kile tulichokiita udalali

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *