Masanja Kadogosa

TRC YAJIVUNIA UBORA WA MIUNDOMBINU

 • Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania TRC Masanja Kadogosa amesema shirika lake limepunguza ajali kubwa za treni kwa asilimia miamoja katika kipindi cha miaka mitatu na nusu na kwamba wanakusudia kuziondoa kabisa hata ajali ndogo kwa kuimarisha miundombinu ya reli.
  Muonekano wa mradi wa Reli ya Kisasa
  Muonekano wa mradi wa Reli ya Kisasa yenye Kiwango cha Kimataifa (SGR) unaotekelezwa na Kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki katika eneo la Karume Jijini Dar es Salaam.
 • Bw. Kadogosa alisema hatua hiyo inatokana na kuimarisha miundombinu ya Reli, Ukarabati wa Mabehewa na usimamizi wa usalama wa reli kazi kazi ambayo imefanywa na Rais Dkt John Pombe Magufuli kutokana na kutoa zaidi ya shilingi Bilioni 3 za kuimarisha miundombinu ya reli inayosimamiwa na TRC.
 • Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kufungua mafunzo ya usalama katika uendeshaji wa shughuli za Reli kwa Wafanyakazi wa TRC, Mkurugenzi Mkuu huyo wa TRC alisema Serikali imekuwa ikiwawezesha kwenye uboreshaji wa miundombinu na sasa wameweza kudhibiti ajali  kwa kusimamia kwenye maeneo yote kuanzia upakiaji wa Abiria na mizigo, usalama wa njia za Reli pamoja na kuimarisha maeneo yaliyokuwa yakisababisha ajali za mara kwa mara.
 • “Sisi TRC hatutegemei kuwepo kwa ajali kubwa tena kwenye eneo letu, na hata hizi ndogo zilizopo zinazotokana na uzembe wa baadhi ya wafanyakazi tunaziondoa, tumeondokana na ajali hizi kwa sababu tumeimarisha miundombinu yetu yote na sasa tunatoa mafunzo ya usalama kwa wafanyakazi ili kuhakikisha tunaziondoa changamoto zote, tunamshukuru Mheshimiwa Rais Magufuli kwani fedha alizotoa zimefanikisha mambo haya” alisema Kadogosa.
WAZIRI MKUU
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (mwenye miwani )akikagua ujenzi wa reli ya kisasa.
 • Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha usalama wa reli na ulinzi TRC Mhandisi Adolfina Ndyetabula alisema usalama umeimarika na kuwataka wananchi kuitumia reli hiyo kwa ajili ya usafiri wa Abiria na mizigo.
 • “Huduma za Reli inayosimamiwa na TRC ni salama na tumeimarisha ulinzi, naomba wananchi tumieni huduma hizi” alisema Mhandisi Ndyetabula.
 • Nae Mkaguzi wa ishara,mawasiliano na umeme Wandema Mtambalike alisema suala la mawasiliano katika usafiri wowote duniani ni muhimu na kuongeza kuwa kwao yameleta manufaa makubwa ya kuondoa ajali za treni.
 • Mafunzo hayo ya wafanyakazi wa TRC yalihusisha idara za Ukaguzi wa Treni na njia yake, Ulinzi na Usalama, Umeme, ubadilishaji wa njia za treni, mafundi pamoja na watoa huduma kwenye reli hiyo.
Ad

Unaweza kuangalia pia

UKARABATI WA KIVUKO CHA MV. PANGANI II WAKAMILIKA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *