HAKUNA SIKUKUU KWENYE KAZI ZA UMEME – WAZIRI KALEMANI

  • Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amewaagiza amewaagiza wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini kuendelea na kazi katika maeneo yao kwa siku zote zikiwemo sikukuu.
  • Alitoa maagizo hayo Aprili 18, 2019 Kongwa, Dodoma alipokuwa akikagua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini; ambapo pia aliwasha umeme katika vijiji vya Ngonga na Mjini Mashariki B.
  • WAKA-2
    Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati), akikata utepe kuashiria uwashaji rasmi wa umeme katika Kijiji cha Mjini Mashariki B, kilichopo wilayani Kongwa, alipokuwa katika ziara ya kazi, Aprili 18, 2019. Kulia kwake ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai.
  • “Wakandarasi, najua kuna sikukuu lakini hakuna sikukuu kwenye kazi za umeme. Jipangeni na magenge yenu. Mameneja na vibarua muendelee na kazi. Hakuna Pasaka kwenye umeme. Umeme ni usalama na umeme ni uhai,” alisema.
  • Aidha, Waziri pia alimwagiza Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Umeme Vijijini Kongwa, kuwaunganishia umeme wananchi wa kijiji cha Ngonga ambao nyumba zao zimerukwa.
WAZIRI
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani, akiwagawia bure vifaa cha Umeme Tayari (UMETA), wakazi wa Kijiji cha Mjini Mashariki B, wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma ili waweze kuunganishiwa umeme pasipo kuingia gharama za kutandaza nyaya. Waziri alikuwa katika ziara ya kazi, ambapo aliwasha rasmi umeme katika kijiji hicho, Aprili 18, 2019.
  • “Sitaki kuona nyumba haina umeme. Nyumba hizi zote mzipelekee umeme. Mmeziruka mkidhani ni za hovyo-hovyo, hakuna nyumba ya hovyo. Nawapa hizi UMETA (Vifaa vya Umeme Tayari), kesho muwaunganishie umeme,” alisisitiza Waziri.
  • Akihamasisha kuhusu matumizi ya UMETA, Waziri Kalemani aliwataka viongozi mbalimbali wa Halmashauri za Vijiji na Wilaya kuhakikisha wanatumia kifaa hicho katika Taasisi za Umma ambazo majengo yake hayana vyumba vingi ili kupunguza gharama za kutandaza nyaya za umeme.
W
Sehemu ya umati wa wananchi wa Kijiji cha Ngonga, wilayani Kongwa, Mkoa wa Dodoma, wakimsikiliza Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani) na kushangilia alipowaahidi kuwa serikali itasambaza umeme katika vitongoji vyote vya kijiji hicho. Waziri alikuwa katika ziara ya kazi, ambapo aliwasha rasmi umeme katika kijiji hicho, Aprili 18, 2019.
  • Aidha, aliwahamasisha wananchi wenye nyumba zenye vyumba vichache (visivyozidi vinne) kutumia vifaa hivyo ili kuepukana na gharama za kutandaza nyaya za umeme.
  • Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kulipia gharama za kuunganishiwa umeme kwenye makazi yao ambazo ni shilingi 27,000 kwa wananchi wa vijijini.
  • “Siyo lazima ulipe yote kwa mkupuo. Unaweza kulipia kidogo kidogo hadi ukafikisha 27,000 na TANESCO watakuunganishia umeme.”
  • Katika ziara hiyo, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Tanzania, ambaye ndiye Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai, alitoa salamu za shukrani kwa serikali kwa kuwapelekea wananchi wake umeme kwa ajili ya maendeleo yao.
  • “Nasimama kwa niaba yenu (wananchi), kutoa shukrani nyingi kwa serikali, kwa será hii nzuri ya kutuletea umeme. Umeme ni maendeleo, umeme ni maisha, umeme ni uhai. Kinachotakiwa sasa ni tuutumie umeme huu.”
  • Aidha, Mheshimiwa Ndugai alimpongeza Dkt. Kalemani kwa kuwa Waziri wa kwanza tangu Tanzania ipate Uhuru, kufika katika Kijiji cha Mjini Mashariki B, kutekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, kwa kuhakikisha wananchi wanapelekewa huduma za maendeleo.
  • Waziri aliambatana na wataalamu mbalimbali kutoka wizarani, TANESCO  na REA.
Ad

Unaweza kuangalia pia

SPIKA WA BUNGE AZINDUA JENGO LA MAHAKAMA WILAYA YA KONDOA

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Mb) leo azindua …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *