- Sserikali imesema kuwa katika mwaka wa fedha 2016/17 hadi 2017/18 ilikusanya kodi ya ongezeko la thamani(VAT) ya kiasi cha Sh. Bilioni 5.5 kwenye bidhaa ya taulo za kike ‘Sanitary Pads’ zilizoingizwa nchini kabla ya kodi hiyo kuondolewa Juni mwaka jana.
- Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum(Chadema), Upendo Peneza.
- Katika swali lake, Peneza alitaka kujua katika mwaka wa fedha 2016/17 na 2018/19 serikali ilikusanya kiasi cha kodi ya asilimia 18 kwa taulo za kike ’Sanitary pads’ zote zilizotengenezwa hapa nchini na zilizoingia kabla ya kodi ya VAT kuondolewa.
- Akijibu swali hilo, Dk.Kijaji alisema katika mwaka wa fedha 2016/17 serikali ilikusanya VAT ya kiasi cha Sh. Bilioni 3.01 na Sh.Bilioni 2.54 kwa mwaka wa fedha 2017/18 kwenye bidhaa ya taulo za kike zilizoingizwa nchini.
- Alisema pia zile zilizozalishwa hapa nchini kabla ya kodi hiyo kuondolewa Juni, 2018.
- Katika swali la nyongeza, Mbunge huyo alihoji japokuwa kodi zimeondolewa kwenye taulo ya kike bado bei ipo juu je ina mpango gani kusimamia suala hilo ili bei zishuke.
- Dk. Kijaji alisema serikali ipo kwenye soko huru kwa bidhaa zote na kwamba haijashindwa kusimamia na ndio maana baada ya kuondoa kodi wameendelea kupokea maoni.
- Kadhalika, alisema utafiti unafanyika na wameenda nchi za Afrika Kusini, Botswana na Kenya ambazo walifanya hivyo lakini waligundua hatua hiyo haiwezi kuleta matokeo chanya.
- “Hivyo tunatakiwa kuhakikisha wanapewa taulo hizo bila kuhusishwa na kodi, tutafanya utafiti na tukijiridhisha kama watoto wetu wanaweza kupewa hivyo alivyotaka Mbunge tutaleta ombi maalum bungeni,”alisema.
Ad