- Serikali ya awamu ya tano imeendelea kutekeleza kwa vitendo ahadi yakeya kutoa fursa za Ajira kwa Watanzania wenye sifa, ujuzi na elimu katikag ngazi mbalimbali kadri ya mahitaji kwa lengo la kuongeza rasilimaliwatue Serikaliniili kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wananchi.
- Kati ya mwezi Machi na Aprili, 2019 zaidi ya nafasi wazi za kazi 1,666 zimetangazwa na Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Akiongea na wadau mbalimbali waliomtembelea ofisini kwake , Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw. Xavier Daudi amesema kuwa nafasi hizo ambazo mchakato wake upo katika hatua mbalimbali ni kwa ajili ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) nafasi 338, madereva 851 kwa ajili ya Wizara, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi nyingine za Serikali, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) nafasi 50, Mamlaka ya Viwanja vya ndege nafasi 119, Mamlaka ya mafunzo yaufundi stadi (VETA) nafasi 43, Chuo cha Taifa cha Usafirishaji nafasi 26, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) nafasi 25 na Chuo cha Elimu ya Biashara nafasi 19.
- Aliongeza kuwa nafasi nyingine ni kwa ajili ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nafasi 16, Wizara ya Afya nafasi 14, Wakala wa huduma za misitu nafasi 11, Shirika la Elimu Kibaha nafasi 9, Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) nafasi 6, Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) nafasi 5,
- Bohari Kuu ya Dawa (MSD) nafasi 3, Mamlaka ya Uendelezaji wa Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KADCO) nafasi 2, Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) nafasi 2, Taasisi ya Utafiti wa Chai (TRIT) nafasi 1, Wakala wa Umeme Vijijini (REA) nafasi 1, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Rufaa ya Ununuzi wa Umma (PPAA) nafasi 1, Hospitali ya Benjamini Mkapa nafasi 1, Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi (MUHAS) nafasi 1, Wakala wa Ndege za Serikali nafasi 1 na Taasisi ya Bahari Dar es Salaam nafasi 1.
- Aidha matangazo hayo yote utekelezaji wake uko katika hatua mbalimbali kulinganana tarehe za kila tangazo.
- Daudi aliongeza kuwa jumla ya nafasi wazi za kazi 146 za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ambazo usaili wake ulifanyika mwezi machi, majina ya waombaji kazi waliopangiwa kituo cha kazi yanatarajiwa kutolewa hivi karibuni.
- Katibu huyo amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano ni Serikali inayolenga kuwa na watu wenye sifa stahili ili kuiwezesha Tanzania kufikia kwenye uchumi wa kati kwa haraka na ndio maana imeendelea kutoa vibali
- vya ajira katika maeneo mbalimbali ili kuongeza rasilimaliwatu katika kusukuma utekelezaji wa mipango na mikakati mikubwa ya Serikali kwa faida ya Taifa.
- Bwana Daudi amefafanua kuwa kuwa ofisi yake imeendelea kubuni mifumo mbalimbali ya TEHAMA ili kuongeza ufanisi wa kazi. Mifumo hiyo mipyaimesaidia kurahisisha uendeshaji wa mchakato wa ajira kwa haraka kwakuzingatia kuwa idadi ya waombaji kazi ni kubwa hivyo pamoja na rasilimaliwatu aliyokuwa nayo lakini matumizi ya mifumo ya TEHAMA hasa ‘recruitment portal’ imeendelea kurahisha mchakato wa ajira kwa kila nafasia za kazi zinapotangazwa.
- “Niwahakikishie kuwa tumeendelea kuboresha huduma zetu za uendeshajiwa mchakato wa ajira kwa kubuni na kuboresha mfumo wa upokeaji wamaombi ya kazi “recruitment portal” mfumo wa kupangia watu kazi kupitia kanzidata (Placement Management Information System).
- Mifumo hii imeongeza uwazi zaidi kwa wateja na wadau wetu kuliko hapo awali, Shabaha yetu ni kufanya kazi kwa malengo hasa kwa kutumiamifumo hii kupata watumishi bora kwa haraka ili kuongeza nguvu yarasilimaliwatu kwa waajiri na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi” alieleza Daudi.
Ad