- Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe amekitaka kikosi kazi kinachojihusisha na uandaaji wa mpango mkakati wa kuendeleza uzalishaji wa zao la mpunga nchini kuhakikisha kinaanda rasimu itakayowezesha uzalishaji wa zao hilo kukuwa mara mbili zaidi kutoka tani milioni 2.2 hadi kufikia tani 4.5 ifikapo 2030.
- Akizungumza na wataalam hao na wadau kutoka taasisi binafsi katika Katibu Mkuu Mtigumwe amesema kufuatia wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuanzisha mpango mkakati wa kuendeleza zao la mpunga yaani National Rice Development Strategy (nrsd) 1 mwaka 2008 kuwa na matokeo chanya ya kuongeza uzalishaji wa mpunga kutoka tani laki 899,000 hadi kufikia tani milioni 2.2 mwaka 2018 ambapo ili kukuza zaidi uzalishaji imeanzishwa nrds 2 itakayokwenda mpaka mwaka 2030 huku lengo likiwa ni kufikia tani za mpunga milioni 4.5…
- “Mpango huu utatekelezwa kwa muda was miaka 12 kuanzia mwaka 2018 had I mwaka 2030 na tayari maandalizi Yake yalianza mwaka 2018 kwa kuanzia kuainishwa takwimu zinazohitajika” amesema Mtigumwe.
- Mwenyekiti wa kikosi kazi hicho Joseph Lubiloh, amesema kuwa matarajio waliyonayo mara baada ya kukamilika kwa mpango wa awamu ya pili na hadi sasa kikosi hicho kimefanikisha kukusanya takwimu kamili za kufanikisha mpango huo huku wadau wengine wakifafanua mipango iliyopo katika kufanikisha mpango huo kuwa ni kushirikiana na serikali kukamilisha juhudi hizo.
Ad