- Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameupongeza Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kazi kubwa inayofanya.
- Hayo ameyasema kwenye mkutano wa hadhara mkoani Mbeya kwenye viwanja vya Ruanda Nzove wakati akizungumza na wananchi muda mfupi baada ya kuzindua jengo la NHIF Tower Mbeya ambalo litatumika kwa ajili ya kuhudumia wanachama pamoja na kitega uchumi.
- “Leo nimepata heshima ya kufungua jengo zuri sana la NHIF na nimpongeze sana Mwenyekiti wa Bodi Mama Makinda ambaye aliona umuhimu wa kujenga jengo hili huku ambalo ni zuri sana hakika alitambua umuhimu wa Mbeya na kilichonifurahisha zaidi ni kusikia jengo lina wapangaji zaidi ya asilimia 91,” alisema Mhe. Rais.
- Kutoka na hayo, Mheshimiwa Rais alitoa pongezi kwa Watendaji wa Mfuko kwa kazi kubwa wanayofanya lakini pia akautaka uongozi kujielekeza katika uwekezaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba ili kuboresha zaidi huduma za matibabu.
- “Majengo ni mazuri lakini tusiendeleze sana kujenga jielekezeni kujenga viwanda vya madawa na vifaa hospitalini lakini kwa hili nakupongeza sana na sijilaumu kukuteua naomba unipelekee pongezi hizi kwa watendaji wa NHIF,” alisema Rais.
- Alitumia pia fursa hiyo kuwaomba watanzania kujielekeza katika kujiunga na Nhif ili waweza kupata huduma kupitia mfumo wa Bima ya Afya.
Ad