Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

WAZIRI MKUU AAGIZA MABANGO YA UTALII YAWEKWE KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIA

  • Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameuagiza uongozi wa bodi ya KADCO uhakikishe unaweka mabango ya kielektroniki yenye kuonesha vivutio vya utalii kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).
  • “KADCO na Wizara ya Maliasili na Utalii, shirikianeni kuweka utaratibu wa kutangaza vivutio vyetu vya utalii hasa wanyama kwenye viwanja vyote vya ndege. Tunazo mbuga, milima, fukwe za bahari na ngoma za makabila mbalimbali, wekeni mabango yanayobadilisha picha.”
  • Screens zenye wanyama wanaobadilikabadilika zinaleta mvuto lakini pia ni fursa ya kutangaza vivutio vyetu. Nimezunguka humu ndani, kuta zote ni nyeupe tu, tumieni fursa hiyo kutangaza tamaduni zetu na vivutio tulivyonavyo,” Waziri Mkuu alimweleza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kilimanjaro Airports Development Company (KADCO), Mhandisi Christopher Mukoma.
  • Alitoa agizo hilo jana mchana (Jumamosi, Aprili 27, 2019) wakati akikagua miundombinu ya uwanja wa ndege wa Kilimanjaro (KIA) mara baada ya kuwaaga watalii 274 kutoka Israeli wanaowawakilisha wenzao 1,000 walioondoka nchini jana kurejea kwao.
  •  Akiwa uwanjani hapo, Waziri Mkuu alikagua eneo la mapokezi, sehemu ya abiria wanaoondoka na wanaowasili, sehemu ya uhamiaji, mashine za kukagua mizigo ya wanaoondoka na wanaowasili, sehemu za kutolea huduma na maduka.
  •  Pia alimwagiza Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji kwenye kiwanja hicho cha ndege, Bw. Filbert Ndege awasiliane na makao makuu yake ili waangalie uwezekano wa kuongeza madirisha ya kutolea huduma za uhamiaji (counters) ili huduma hiyo itolewe kwa kasi zaidi.
  •  “Angalieni cha kufanya, ikibidi eneo hili lipanuliwe na counters nyingine ziongezwe ili kufasttrack utoaji wa huduma hasa msimu ambao watalii wengi huingia nchini.”
  • Pia aliwataka KADCO waboreshe eneo la maegesho ya magari kwa kufanya upanuzi na kujenga maturubai ya vivuli (shades) ili kuyakinga na jua kali magari ya wateja.
Ad

Unaweza kuangalia pia

MATUKIO YA WAZIRI MKUU BUNGENI MJINI DODOMA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *