JUMUIA ZA KIMATAIFA ZAHAKIKISHIWA KUIMARISHWA KWA UHURU WA VYOMBO VYA HABARI,KUKUZA DEMOKRASIA NA HAKI ZA BINADAMU

  • Waziri wa Mambo ya Nje Pro. Palamagamba Kabudi ameihakikishia jumuia za kimataifa kuwa Tanzania itaendelea kulinda uhuru wa vyombo vya habari ambao umejikita katika misingi ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kukuza demokrasia na haki za binadamu kwa mujibu na muktadha wa nchini.
  • Pro. Kabudi ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Balozi Malika James,na kuongeza kuwa  Tanzania ni miongoni mwa nchi chache Barani Afrika na pengine duniani kuwa na vyombo vingi vya habari ambavyo vingi vinamilikiwa na watu binafsi na kwamba itaendelea kuuheshimu uhuru huo huku akivitaka vyombo vya habari navyo kuheshimu uhuru na haki za watu wengine.
  • “Tutaendelea kuulinda uhuru wa vyombo vya habari lakini uhuru ambao umejikita katika misingi ya katiba yetu,pia uhuru ambao utaheshimu uhuru na haki za watu wengine”   
  • Kuhusiana na suala la demokrasia Nchini,Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi amesema kuwa Tanzania itaendelea kukuza demokrasia kwa mujibu wa muktadha na mazingira ya Tanzania ambayo huenda ikawa ni tofauti na nchi nyingine ikiwemo kutoruhusu ukabila,udini na ubaguzi wa aina yeyote na kuongeza kuwa vitu hivyo ni muhimu katika kukuza demokrasia ya nchi.
  • “Pamoja na kwamba sisi sote ni Waafrika,ziko nchi zaidi ya 50 huku kila nchi ikifanya na kujiamulia mambo yake tofauti nan chi nyingine hivyo wasitumie vigezo na muktadha wan chi nyingine katika kuitathmini Tanzania.” 
  • Aidha ameongeza kuwa licha ya Tanzania kuhakikisha inaimarisha uhuru wa vyombo vya habari na kukuza demokrasia pia inaimarisha haki za binadamu nchini kwa kutumia taasisi zilizopo na kuruhusu uhuru wa mahakama.

Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI ZUNGU AHUDHURIA MKUTANO WA 7 WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI WA MAZINGIRA NA MALIASILI WA JUMUIA YA AFRIKA MASHARIKI

             

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *