UWEKEZAJI KWENYE MIRADI YA UMEME VIJIJINI UCHAGIZE UKUAJI WA UCHUMI – SIMBACHAWENE

  • Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, George Simbachawene ametoa wito kwa Serikali kuhakikisha kuwa uwekezaji mkubwa unaofanywa katika miradi ya umeme vijijini unachagiza ukuaji wa uchumi kwa kupeleka umeme unaotosholeza mahitaji ya wananchi na kusambaza umeme katika Taasisi za Serikali na kijamii.
  • Simbachawene ameyasema hayo jijini Dodoma, tarehe 4 Mei, 2019 wakati wa kikao kilicholenga kupata taarifa kuhusu mwenendo wa ukusanyaji na utolewaji wa tozo ya mafuta ya petroli kwa ajili ya kugharamia miradi ya umeme vijijini  kwa mwaka 2018/2019.
  • Akizungumza katika kikao hicho kilichohudhuriwa na  Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, Simbachawene alisema, “ Serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hii ya umeme vijijini, hivyo lazima mhakikishe kuwa umeme unaosambazwa unatosheleza mahitaji na si utumike tu kuwasha taa, mtu anapotaka kuanzisha kiwanda au kazi yoyote inayohitaji umeme asikwame, hii itapelekea miradi hii kuleta tija.”
    SUBIRA
    Wataalam kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wizara ya Nishati wakifuatilia kikao kilichohusu kilichohusu mwenendo wa ukusanyaji na utolewaji wa tozo ya mafuta ya petroli kwa ajili ya kugharamia miradi ya umeme vijijini kwa mwaka 2018/2019 kilichofanyika jijini Dodoma.
  • Simbachawene pia aliishauri Wizara ya Nishati kuhakikisha kuwa, wanaendelea kuwashirikisha wawakilishi wa wananchi katika kazi za usambazaji umeme vijijini ili kazi hizo zifanyike kwa ufanisi.
  • Awali, akitoa taarifa kwa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga, alisema kuwa, katika kipindi cha kuanzia Julai 2018 hadi  mwishoni mwa Aprili, 2019, Wakala umepokea fedha za ndani kiasi cha shilingi bilioni 305.56 ambayo ni sawa na asilimia 97.7 ya fedha zilizopangwa kutolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.
Screen Shot 2019-05-06 at 10.11.49 AM
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, George Simbachawene (kulia) na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu wakiwa kwenye kikao kilichohusu mwenendo wa ukusanyaji na utolewaji wa tozo ya mafuta ya petroli kwa ajili ya kugharamia miradi ya umeme vijijini kwa mwaka 2018/2019 kilichofanyika jijini Dodoma.
  • Aliongeza kuwa, kwa upande wa fedha za nje, Wakala huo umepokea kiasi cha shilingi bilioni 87.75 na hivyo kufanya jumla ya fedha zilizopokelewa na Wakala kwa miradi ya umeme vijijini kuwa ni shilingi bilioni 393.31.
  • Akieleza kuhusu utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini, Mhandisi Maganga alisema kuwa, jumla ya vijiji vilivyofikiwa na umeme Tanzania Bara hadi kufikia tarehe 30 Aprili, 2019 ni 6,590 ambayo ni sawa na asilimia 53.7 ya vijiji vyote vya Tanzania Bara.
SUBIRA
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Wataalam kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wizara ya Nishati wakifuatilia kikao kilichohusu kilichohusu mwenendo wa ukusanyaji na utolewaji wa tozo ya mafuta ya petroli kwa ajili ya kugharamia miradi ya umeme vijijini kwa mwaka 2018/2019 kilichofanyika jijini Dodoma.
  •  Aidha, alisema kuwa, jumla ya Taasisi za umma 8,986 zimepatiwa umeme kupitia miradi hiyo ya umeme vijijini  na matarajio ni kuwa hadi kufikia mwezi Julai, 2020,  Vijiji 9,299 ambavyo ni sawa na asilimia 75.7 ya Vijiji vyote vya Tanzania Bara vitakuwa vimefikiwa na umeme.
  • Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amesema kuwa, wadau wa maendeleo ikiwemo Umoja wa Ulaya (AU), Serikali ya Sweden na Serikali ya Norway wana imani na Serikali ya Awamu ya Tano hasa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ndiyo maana wanaendelea kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini.
  • Kuhusu upatikanaji wa vifaa vya umeme vinavyozalishwa ndani ya nchi kama vile nguzo, Mgalu alisema kuwa vifaa hivyo vinaendelea kutolewa kwa wakandarasi na kwamba Serikali inaendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini ili itekelezwe kwa muda uliopangwa.Na Teresia Mhagama
Ad

Unaweza kuangalia pia

WAZIRI MKUU AMPONGEZA BONDIA SALIM MTANGO ALIYESHINDA MKANDA WA DUNIA WA UBO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *