KAZI YA KUSIMIKA MIFUMO NDANI YA TERMINAL III IMEKAMILIKA KWA ASILIMIA 96.8

  • Tanzania mpya imedhihirishwa na Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (Terminal 3)  katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
  • Akizungumza na Idara ya Habari Maelezo hivi karibuni Msimamizi wa mradi  wa ujenzi wa uwanja huo kutoka Wakala wa Taifa wa Barabara TANROADS, Mhandisi Barton Komba amesema:
  • “Jengo la tatu la Abiria limesanifiwa kwa viwango vya Kimataifa vya daraja C vya Usafiri wa Anga – IATA. Hivyo linatarajiwa kwa sasa kuwa  kituo kikuu cha usafiri wa anga na kuleta tija kwa Tanzania”.
  • Mhandisi  Komba ameongeza kwa kusema, asilimia 70 ya gharama  ya  mradi zimetumika kwenye usimikaji wa miundombinu ya mifumo  maalum ndani ya jengo (airport special systems).

AIPORT 2-01

 
  • “Nasema ukizungumzia  uwanja wa ndege, unazungumzia usalama wa abiria na mizigo, gharama iliyotumika katika usalama wa eneo la ndani ya jengo  (Mechanical Eletrical Plumbing – MEP) pamoja na kufanyia kazi  eneo la uhamiaji ambapo ni zaidi ya asilimia 70  ya mradi, mitambo ndio imechukua sehemu kubwa ya gharama.” Aidha, Mhandisi Komba amesema kuwa, katika eneo hilo sehemu ya  uhamiaji  kumefungwa madawati  10  yenye  sehemu za kufanyia kazi   40  zenye   uwezo wa kuhudumia abiria arobaini wanaowasili au kuondoka kwa wakati mmoja.
  • Mhandisi Komba amesisitiza kwa kusema kuwa kwa abiria ambao wanaotumia hati za kusafiria za kieletroniki  (E Passport) hawatalazimika  kupita  kwenye huduma za uhamiaji bali kwenye lango  la kieletroniki ( E-Gate) ambapo watahakiki hati zao za kusafiria na alama za vidole.
  • Pia, kwa upande wa ukaguzi wa mizigo (Baggage Handling System HBS) umesimikwa  mfumo wa kisasa wenye uwezo wa kukagua mizigo katika madaraja matano tofauti  pamoja na  mashine za kukagua mizigo midogo ya mkononi . Ameainisha Mhandisi Komba

AIRPORT 3-01

  • Komba amesema kuwa daraja la kwanza mzigo utaangaliwa kwa mashine (scanner) ili kubaini taswira ya kitu kilichomo ndani ambapo daraja la pili mzigo huo utachunguzwa tena kwa kutumia mashine (scanner) zenye nguvu zaidi ya kuona kwa kina. Daraja la tatu mzigo utachunguzwa kwa kutumia mashine zenye uwezo wa kuchanganua picha ya mzigo iliyoonekana kwenye daraja la pili kwa vipande mia moja tofauti (3 Dimention).  Hatua itakayofuata ni mzigo utaingia daraja la nne sehemu ya wataalamu wenye uwezo wa kutasiri picha iliyoonekana katika madaraja yote yaliyotangulia.
  • Mhandisi Komba amesema, endapo mzigo hautakuwa na dosari ukifika daraja la nne utapata  kibali na hivyo kuingizwa kwenye ndege.  Aidha, mzigo wenye dosari utaingia daraja la tano ambapo hatua za kisheria zitachukuliwa  na vyombo vya usalama.

AIRPORT 4-01

  • Akifafanua Mhandisi Komba ameeleza kuwa eneo la kupokea mizigo lenyewe linayo mikanda minne yenye urefu wa mita 95, ukiwemo mmoja kwa ajili ya mizigo hatarishi inayotoka sehemu zisizokuwa na uhakika wa usalama kuingia kwenye nchi yetu. Akielezea miundombinu mingine Mhandisi Komba amesema “Miundombinu iliyosimikwa kwa viwango vya kimataifa ndani ya jengo hili ni mifumo ya tahadhari ya zima moto, utandazaji wa nyaya , ufungaji wa lifti na escalator pamoja na kazi nyingine za ndani  ambazo kwa ujumla wake zimekamilika kwa asilimia 96.8”.
  • Kwa mujibu wa Mhandisi Komba, eneo la maegesho ya ndege na viungio vyake lenye ukubwa  mita  za mraba 227,000, limekamlika kwa  asilimia 99.9 na kwamba ndege 19 za daraja C ambazo ni ndogo na ndege 11  za daraja E ambazo ni kubwa kama vile Boieng 787, Dreamliner   zinaweza kuegeshwa kwenye eneo hilo. Tofauti ya ndege za daraja C na daraja E pia inatokana na urefu wa ndege, upana wa mabawa yake na vilevile ukubwa na idadi ya abiria.

AIRPORT 5-01

  • Amesema, Mhandisi Komba kuwa, kazi nyingine iliyokamilika na kuupa uwanja huu muonekano wa kimataifa ni usimikaji wa vivuko vya abiria 12 (Passanger Boarding Bridges) pamoja na ujenzi wa barabara  za viungio kuingia na kutoka kwenye maegesho ya ndege. Kukamilika kwa mradi huu kunatarajiwa kuwa chaguo la ndege nyingi zinazoruka kwenda nchi za Afrika na bara Asia na Ulaya.
  •  Eneo la nje ya jengo ambalo ni  maegesho ya magari ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 98.6 na ipo nafasi ya kuegesha magari 2,000 kwa ajili ya abiria wanaokuja na kuondoka nchini. Katika eneo hili  imesimikwa mifumo ya kupoozea hewa na mifumo ya maji ya mvua na maji taka. Aidha, taa nyingi zimefungwa kwenye maegesho ya magari, jenerata 7 kwa ajili ya dharura kila moja ikiwa na uwezo wa 2MVA ili kuhakikisha huduma zinapatikana wakati wote hata inapotokea hitilafu ya umeme.
  • Akielezea historia ya uwanja wa ndege wa Kimatafa wa Julius Nyerere Mhandisi Komba amesema kuwa, ujenzi wa jengo la tatu la abiria ni mwendelezo wa majengo  mawili ya abiria ya zamani yaani Terminal 1 na Terminal 2. Kilianza kufanya kazi mwaka 1959 kikiwa na jengo moja la abiria lenyw uwezo wa kuhudumia abiria laki 5 kwa mwaka na barabara moja ya kuruka na kutua ndege.
 
Ad

Unaweza kuangalia pia

SERIKALI INATARAJIA KUJENGA MINARA 5 YA MAWASILIANO WILAYANI MAFIA

Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Injinia Atashasta Nditiye (Mb.) amezindua mnara wa Mawasiliano …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *