- Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imeyaagiza makampuni ya Premium Agrochem, OCP na Export Trading Group (ETG) kuhakikisha kwamba ifikapo Julai, 2019 kampuni hizo ziwe na ghala za kuhifadhia mbolea na mawakala wa kusambaza katika mikoa inayotumia mbolea kwa wingi ukiwemo mkoa wa Katavi ili kuondoa changamoto ya upungufu wa mbolea kwa wakulima katika maeneo hayo.
- Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Mb) ameyasema hayo leo tarehe 10 Mei 2019 wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu Mhe Taska Restituta Mbogo aliyetaka kufahamu kuwa serikali ina mpango gani wa kusambaza mbolea kwa wakati katika mkoa wa Katavi.
- Alisema kuwa Serikali inatumia Mfumo wa Ununuzi wa mbolea kwa pamoja Bulk Procurement System – BPS kuagiza mbolea ya kupandia (DAP) na mbolea ya kukuzia (UREA), Mfumo huo unawezesha upatikanaji wa mbolea kwa wakati na kwa bei nafuu na kudhibiti upandishaji wa bei za mbolea kiholela.
- Mhe Mgumba aliongerza kuwa Serikali inakamilisha zabuni ya kuingiza mbolea tani 280,000 ambapo tani 170,000 ni mbolea ya kupandia na tani 110,000 ni mbolea ya kukuzia kwa ajili ya msimu wa 2019/2020 kupitia mfumo wa BPS.
-
Alisema, Mbolea hiyo inatarajiwa kufikishwa hapa nchini mwezi Agosti, 2019 na kusambazwa kwa wakulima wa mkoa wa katavi na maeneo mengine nchini kabla ya mwezi Septemba 2019. Vile vile, ziada ya mbolea iliyopo nchini inaendelea kusambazwa katika maeneo mbalimbali kulingana na msimu ambapo hadi tarehe 30 Machi, 2019 kulikuwa na tani 147,913 za mbolea.
-
Aidha, Serikali inatumia Mfumo wa Ununuzi wa mbolea kwa pamoja Bulk Procurement System – BPS kuagiza mbolea ya kupandia (DAP) na mbolea ya kukuzia (UREA). Mfumo huo unawezesha upatikanaji wa mbolea kwa wakati na kwa bei nafuu na kudhibiti upandishaji wa bei za mbolea kiholela.
- Serikali inakamilisha zabuni ya kuingiza mbolea tani 280,000 ambapo tani 170,000 ni mbolea ya kupandia na tani 110,000 ni mbolea ya kukuzia kwa ajili ya msimu wa 2019/2020 kupitia mfumo wa BPS. Mbolea hiyo inatarajiwa kufikishwa hapa nchini mwezi Agosti, 2019 na kusambazwa kwa wakulima wa mkoa wa katavi na maeneo mengine nchini kabla ya mwezi Septemba 2019.
- Kadhalika, Mhe Mgumba alisema kuwa ziada ya mbolea iliyopo nchini inaendelea kusambazwa katika maeneo mbalimbali kulingana na msimu ambapo hadi tarehe 30 Machi, 2019 kulikuwa na tani 147,913 za mbolea.
- “Serikali imelielekeza Shirika la Reli Tanzania kutoa kipaumbele cha kusafirisha mbolea ili kusafirisha mbolea nyingi kwa wakati mmoja na gharama nafuu ili kumfikia mkulima kwa wakati na bei nafuu” Alikaririwa Mhe Mgumba na kuongeza kuwa
- Serikali inakusanya mahitaji ya mbegu bora na viuatilifu kutoka katika mikoa ili kuhamashisha kampuni na wafanya biashara kupeleka pembejeo hizo kwa wakulima kabla ya msimu wa kilimo kuanza na wakati wa mauzo ya mazao.(Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo – Dodoma)
Ad