- Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe Mh, Edward Haule mei 06/2019 aliongoza Jopo la Viongozi wa kata mbili za Madope na Lupanga pamoja na Wananchi wa Kata hizo kuchimba Barabara ya kuunganisha Vijiji Jirani katika Kata hizo.
- Barabara hiyo yenye urefu wa zaidi ya kilometa sita licha ya kupita kwenye eneo lenye mlima lakini wananchi hao wameungana kuichimba kwakutumia Vifaa vya mikono kuambaa pembeni mwa mlima huo.
- Akizungumza na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Lusala kata ya Lupanga na Kijiji cha Luvuyo kata ya Madope Vijiji ambavyo vinaunganishwa kwa Barabara hiyo, Mh.Edward Haule amewaomba wananchi kuendelea kuungana kwa pamoja ili wakamilishe barabara hiyo kwa wakati.
- Aidha amewapongeza wananchi pamoja na madiwani wa kata mbalimbali wilayani Ludewa kwa kujitokeza kwa wingi katika shughuli hiyo na kuwataka kuendelea kuungana na wananchi katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa taifa.
- Policapy Mlelwa ni Diwani wa kata ya Madope amepongeza Juhudi za Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kwa kujituma kufungua mtandao wa Barabara tofauti wilayani humo, huku akikiri wazi kuwa Mwenyekiti huyo ni mfano wa kuigwa na Viongozi wengine.
- Kwa upande wao wananchi wa Vijiji Vinavyounganishwa na mtandao huo wa Barabara wamepongeza Juhudi za Halmashauri ya wilaya ya Ludewa kupitia Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo mh.Edward Haule kwa kuwaunganisha wananchi wa Vijiji mbalimbali kupitia mtandao wa Barabara.
- Zoezi hilo la uchimbaji wa Barabara litaendelea tena siku ya Jumatatu Mei 13 /2019 huku Wadau wa maendeleo kutoka ndani na nje ya wilaya ya Ludewa walioguswa na wenye nia ya kuunga mkono juhudi za Wananchi na Serikali wanaombwa kuchangia zoezi hilo.
Ad