- Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira jijini Mwanza (MWAUWASA) imesaini mkataba na mkandarasi kampuni ya BENNET Contractors, kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa maji kwa wakazi wa Kata ya Nyashimo, Wilaya Busega mkoani Simiyu.
- Mkataba huo umesainiwa Mei 10, 2019 na kushuhudiwa na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa Simiyu, Antony Mtaka aliyebainisha kwamba kukamilika kwa miradi mbalimbali ya maji wilayani Busega, kutaongeza idadi wananchi wanaofikiwa na mtandao wa maji safi na salama kutoka asilimia 39 za sasa hadi asilimia 79.
- Mkurugenzi wa MWAUWASA, Mhandisi Antony Sanga amesema utekelezaji wa mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 1.8 ni sehemu ya ahadi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati akizungumza na wakazi wa Kata ya Nyashimo.
- Naye Mkurugenzi wa kampuni ya BENNET Contractors, Sabatho Boaz ameahidi kukamilisha mradi huo kwa ubora na kwa muda wa miezi 15 kama mkataba unavyoelekeza ili kuwaondolea wananchi wa Kata ya Nyashimo adha ya upatikanaji wa maji safi na salama.Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Ad