Prof. Lawrence Museru akikabidhiwa bango leo na Rais wa Rotary Club Oyster bay jijini Dar es Salaam, Vikash Shah.

MUHIMBILI YAPOKEA VIFAA TIBA VYA KUTIBU SARATANI YA MACHO

  • Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imepokea msaada wa mashini za kutoa tiba ya saratani macho kwa watoto bila kuyaondoa zenye thamani ya shilingi milioni 170 kutoka Rotary Club Oyster bay jijini Dar es Salaam.
  • Msaada huu utawanufaisha watoto wengi wanaofikishwa hapa Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa huduma ya saratani ya macho kutoka mikoa mbalimbali nchini.
MH 1-01
Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza baada kupokea msaada wa vifaa vinavyotumika kutoa huduma ya saratani ya macho kutoka Rotary Club Oyster bay jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto kwake ni Rais wa Rotary Club Oyster bay ya Dar es Salaam, Vikash Shah na Mkurugenzi wa Mradi, Kripa. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Upasuaji wa Muhimbili, Dkt. Baruani Sufiani na Dkt. Anna Sanjiwa wa Muhimbili.\
  • Akizungumza baada ya kukabidhiwa msaada, Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru ameishukuru Rotary Club kwa kuwa vifaa hivi vitatoa tiba sahihi kwa watoto mwenye saratani ya macho bila kufanyiwa upasuaji wa kuyaondoa.
  • Prof. Museru amesema watoto wenye seratani ya macho watakuwa wakipatiwa huduma ya mionzi baridi na moto.
  • “Huu ni msaada mkubwa kwani vifaa vitasaidia kutoa tiba sahihi kwa watoto wenye matatizo ya saratani ya macho. Muhimbili tuna zaidi ya watoto 100 wanaougua saratani mbalimbali, hivyo tuna kazi kubwa ya kuwapatia huduma bora ya afya,” amesema Prof. Museru.
  • Pia, Mkurugenzi ameipongeza shirika lisilo la kiserikali la Tumaini la Maisha Tanzania (TLM) kwa kutoa huduma bure ya matibabu,malazi na chakula kwa watoto wenye saratani ya aina mbalimbali.
MH 3-01
Prof. Museru wa Muhimbili na Rais wa Rotary Club, Vikash Shah wakiwa katika picha ya pamoja na wataalam wa MNH na wawakilishi wa Rotary Club ya Oyster bay jijini Dar es Salaam.
  • Mkurugenzi wa Mradi wa Rotary Club ya Oyster bay, Kripa amesema wametoa msaada kwa ajili ya kuboresha huduma ya matibabu kwa watoto wenye saratani ya macho.
  • Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Macho, Dkt. Anna Sanyiwa wa Muhimbili amesema vifaa hivi ni vya kisasa na kwamba vinatumiwa na nchi mbalimbali duniani kutoa tiba ya saratani ya macho.
  • “Ni vifaa muhimu kwa tiba ya saratani ya jicho. Vifaa hivi vinatusaidia kuondoa vivimbe kwenye macho au jicho bila kufanya upasuaji wa kuondoa jicho la mgonjwa mwenye saratani. Kabla ya kupata vifaa, tulikuwa tunalazimika kuondoa jicho kwa mgonjwa,” amefafanua Dkt. Anna.
  • Amesema endapo watoto wenye saratani ya macho wakifikishwa hospitali mapema watatibiwa bila macho au jicho kuondolewa kwa kutumia vifaa vilivyokabidhiwa.
  • Vifaa vilivyopokelewa  ni mashini mbili ya mionzi ya moto, mashini moja ya mionzi baridi na kamera mbili.
Ad

Unaweza kuangalia pia

ONGEZENI KASI YA KUWAHUDUMIA WANANCHI – DKT. CHAULA

Watumishi wa afya nchini wametakiwa kuongeza kasi ya kuwahudumia wananchi kwenye vituo vya kutolea huduma …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *