Eneo la kimila linalojulikana kama Oreteti Loongaik ambalo ndiyo mahali Wazee wa kimila wa kabila Maasai hukutana na kufanya mashauri mbalimbali yanayohusiana na kabila hilo. Eneo hilo lipo ndani ya Chuo cha Ufundi Arusha .(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,ARUSHa.

MAKATIBU WAKUU WA HABARI NA ELIMU WAKUTANA KUJADILI SULUHU YA ENEO LA KIMILA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA.

  • Makatibu Wakuu wa Wizara ya Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi na Katibu Mkuu Wizara ya  Elimu , Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo pamoja na Kaimu Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha Dkt. Masudi Senzia wamekutana na Viongozi wa Wazee wa Kimasai ili kupata suluhu la eneo la kimila  maarufu kama Oreteti Loongaik lililopo ndani ya chuo hicho.
  • Kikao hicho kimefanyika leo Jijini arusha  katika  Ofisi za Kaimu Mkuu wa Chuo Cha Ufundi Arusha agenda  kuu zikiwa ni kuongezewa eneo ili wazee wa kimila waweze kufanya shughuli zao za mila kwa nafasi, kupewa kibali cha kujenga nyumba kwa ajili ya kujihifadhi wakati wa mvua pamoja na kuwa na geti la kuingilia tofauti na geti la chuo.
KM
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo akiongea na Wazee wa Kimila wa kabila la Wamasai wakati wa kikao cha usuluhishi kuhusu eno la kimila maarufu kama Oreteti Loongaik lililopo katika Chuo cha Ufundi Arusha.
KM
. Mwenyekiti wa Wazee wa Kimasai Bw. Laiza Ole Kisongo akiongea wakati wa kikao cha usuluhishi kuhusu eno la kimila maarufu kama Oreteti Loongaik lililopo katika Chuo cha Ufundi Arusha.
  • Makatibu Wakuu hao walipata wasaa wa kuwasikiliza , kujadiliana pamoja na kutembelea eneo hilo la kimila ili kuweza kuona ni kwa namna gani wanaweza kutoa maamuzi ambayo hayataadhiri upande wowote na hivyo kufikia muafaka mzuri.
KM
. Mwakilishi wa Akina Mama kutoka Jamii ya Kimasai Bibi. Agness John akichangia jambo wakati wa kikao cha usuluhishi kuhusu eno la kimila maarufu kama Oreteti Loongaik lililopo katika Chuo cha Ufundi Arusha.
  •  “Serikali inatambua umuhimu wa kuenzi na kudumisha mila na ndio maana tupo hapa leo ili kuweza kupata suluhisho la kudumu kuhusu eneo hili ambalo limekuwapo tangu enzi na enzi” alisema Bibi. Susan Mlawi.
KM
Viongozi wa Wazee wa Kimila wa kabila la Wamasai pamoja na Makumu Mkuu wa Chuo cha ufundi Arusha Dkt. Erick Mgaya wakiwasikiliza Makatibu Wakuu kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu , Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo (hawapo katika picha) wakati wa kikao cha usuluhishi kuhusu eno la kimila maarufu kama Oreteti Loongaik lililopo katika Chuo cha Ufundi Arusha .
  • Aidha Katibu Mkuu , Bibi. Susan Mlawi aliupongeza uongozi wa chuo kwa kuwaruhusu Wazee hao kuweza kufanya shughuli  za kimila katika eneo hilo na hivyo kusaidia katika kuendeleza utamaduni.
  • Naye Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo aliwataka Wazee hao wa kimila kuendelea kufuata taratibu za kupata kibali kutoka kwa uongozi wa chuo ili kuweza kufanya vikao vyao vya kimila hadi pale suluhisho la kudumu litakapofikiwa.
KM
Eneo la kimila linalojulikana kama Oreteti Loongaik ambalo ndiyo mahali Wazee wa kimila wa kabila Maasai hukutana na kufanya mashauri mbalimbali yanayohusiana na kabila hilo. Eneo hilo lipo ndani ya Chuo cha Ufundi Arusha .(Picha na Lorietha Laurence-WHUSM,ARUSHa.
  • “Mapendekezo yenu ni mazuri nasi tumeyapokea na tunaahidi kuyafanyia kazi  ambapo baada  ya mwezi mmoja tutarudi  tena mahali hapa tukiwa na majibu kutoka kwa viongozi wetu ambao ni Mawaziri wenye dhamana na Wizara hizi mbili” alisema Katibu Mkuu Dkt. Akwilapo.
KM
Katibu Mkuu Wizara ya Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bibi. Susan Mlawi akifafanua jambo wakati wa kikao na Wazee wa Kimila wa Kimasai kilichofanyika leo Katika Chuo Cha Ufundi Arusha (ATC).
  • Kwa Upande wa Mwenyekiti wa Wazee wa Kimasai Bw. Laiza Ole Kisongo ameishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa suala hilo na kuwapa nafasi ya kuweza kujadiliana kwa pamoja ili kufikia muafaka na kujenga taifa lenye umoja na amani.Na Lorietha Laurence-WHUSM, ARUSHA
Ad

Unaweza kuangalia pia

MWANAFUNZI WA MALANGALI AINGIA KUMI BORA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE

#SisiTumeona SISI WATANZANIA TUNAWEZA Hivi sasa watoto wetu wanapata elimu bure bila malipo! ——————————— Matokeo …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *