- Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamwele amefanya ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa jengo jipya la 4 la abiria (Terminal 3) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) leo jijini Dar es Salaam na kuonesha kuridhishwa na usimamizi.
- Akizungumza na waandishi wa habari Kamwele amesema kuwa kasi ya ujenzi huo ni nzuri na hadi sasa uwanja umekamilika na upo katika majaribio na utakabidhiwa rasmi tarehe 29 mwezi huu badala ya tarehe 31 na hiyo ni baada ya uwanja huo kukamilika kwa asilimia kubwa.
- Amesema kuwa majaribio kwa ajili ya uwanja huo wa terminal 3 unaendelea huku akiwahimiza wazawa kutumia fursa ya kutumia nafasi maalumu zilizowekwa kwa ajili ya kuuza chakula (canteen) ili waweze kujiongezea kipato.
- Aidha ameipongeza Mamlaka ya viwanja vya ndege nchini kwa kusimami vyema mradi huo na amemshukuru Rais Dkt. John Magufuli kwa kuleta maendeleo yenye tija kwa kuwa kupitia uwanja huo watalii wengi wanatarajia kuingia nchini huku akieleza kuwa hali ya ulinzi uwanjani hapo ni salama kwa kila mmoja atakaye kuwepo uwanjani hapo.
- Kuhusiana na ujenzi wa daraja la Salender Kamwele amesema kuwa kasi inaenda vyema na barabara ya muda inajengwa na mwisho wa mwezi huu ujenzi rasmi utaanza rasmi.
- Amesema kuwa ujenzi wa daraja hilo lenye mita 1030 umekamilika kwa asilimia 9.5 na tayari mitambo na nguzo zimewasili kwa ajili ya kazi hiyo.
- Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya viwanja vya ndege nchini Mhandisi. Julius Ndyamukama amesema kuwa uwanja wa Terminal 3 una uwezo wa kubeba zaidi ya watu milioni 6 kwa mwaka, kupaki ndege kubwa 13 umekamilika na kazi za majaribio zinaendelea ikiwemo kufunga mitambo kutoka mamlaka za uhamiaji, mabenki, shirika la simu la TTCL na wadau wakubwa katika uwanja huo.
- Amesema kuwa zaidi wa wananchi 2900 ambao ni sawa na asilimia 70 wamenufaika na ajira kupitia mradi huo na ameipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa kasi katika usimamizi wa miradi ya kimaendeleo na kuahidi kuendelea kutekeleza miradi ya namna hiyo kwa wakati.
- Tafiti zinaonesha kuwa Uwanja wa Terminal 1 una uwezo wa kubeba watu laki tano kwa mwaka, Terminal 2 una uwezo wa kubeba watu zaidi ya milioni mbili na nusu kwa mwaka na ujenzi wa uwanja wa terminal 3 unataraji kubeba watu zaidi ya milioni 6 kwa mwaka na umekuja baada uwanja wa terminal 2 kuzidiwa na idadi kubwa ya watu na hii ni kutokana na kukua kwa uchumi na shughuli za kitalii ambapo watu wengi hutumia usafiri wa anga.
- Mradi huo wa ujenzi wa uwanja wa terminal 3 umewekezwa hadi mwaka 2035 kimatumizi huku viwanja vingine 9 vikitarajiwa kujengwa katika Mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Ruvuma na Mara.
Ad
Awali ya yoote namshukuru Mwenyeezimungu kwa ajili ya kutupatia Rais wetu Mpendwa John Pombe Magufuli Mwenyeezimungu Baba tunakushukuru saana.
Pili najifunia kuwa Mtanzania, Watanzania wenzangu tujifunie nchi yetu na tujifunie maendeleo ya nchi yetu tumuunge mkono Rais wetu na wasaidizi wake woote.
Binafsi naona nchi yangu Tanzania yangu Mpya tulipotoka na tulipo ama kweli nyumbani kumenoga kwa kila kitu Watanzania wenzangu wenye umri kuanzia miaka 50 na kupanda juu tunajua tulipotoka na tulipo na tunapokwenda kwa mwendo huu kwa Imani tutaweza Mwenyeezimungu atatuwezesha kila kizuri kina changamoto zake tuwe watulivu kwa ajili ya vizazi vyetu vya baadae Viva Magufuli Viva Watenda Kazi woote Viva Watanzania